title : Azi Shaweji asimamishwa mechi nne Ligi Kuu zenj, Kocha Abrahman Mussa apigwa stop kukaa Benchi
kiungo : Azi Shaweji asimamishwa mechi nne Ligi Kuu zenj, Kocha Abrahman Mussa apigwa stop kukaa Benchi
Azi Shaweji asimamishwa mechi nne Ligi Kuu zenj, Kocha Abrahman Mussa apigwa stop kukaa Benchi
Kocha wa Kilimani Cit y Abrahman Mussa kushoto
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kimempa adhabu ya kumsimamisha kucheza mechi nne beki wa Kilimani City, Aziz Shaweji baada kupatikana na hatia ya kukiuka nidhamu ya michezo katika mechi kati ya Kilimani City na Black Sailors iliyopigwa juzi Jumapili saa 8 za mchana katika uwanja wa Amaan.
Akizungumzia kadhia hiyo katibu mkuu wa ZFA Mohd Ali Hilali “Tedy” amesema Shaweji alipatikana na kosa wakati timu yake ya Kilimani City ilipofungwa 2-0 na Black Sailors ambapo alimzonga Muamuzi wa kati wa mchezo huo Mfaume Ali Nassor.
“Tumepitia CD tukaona Aziz amefanya vitendo visivyokuwa si vya nidhamu, hivyo tumemsimamisha mechi nne”.
Shaweji atazikosa mechi kati ya Kilimani City dhidi ya Jang’ombe Boys itakayopigwa Oktoba 30, Kilimani city na Chuoni ya Novemba 6, Kilimani city dhidi ya Charawe ya Novemba 12 na ya mwisho Kilimani city dhidi ya Zimamoto itakayopigwa Novemba 19.
Wakati huo huo kocha wa Kilimani City Abrahman Mussa nae amesimamishwa kukaa katika benchi hadi pale atakapopeleka vyeti vyake vya ukocha ZFA.
Katibu Tedy amesema wamemsimamisha mpaka wathibitishe cheti chake cha ukocha kama kweli anastahiki kuwa Mwalimu wa Soka kwani katika mchezo kati Kilimani City walipochapwa 2-0 na Black Sailors uliyopigwa juzi Jumapili saa 8 za mchana katika uwanja wa Amaan Mwalimu huyo baada ya kumaliza mchezo alimzonga Muamuzi wa kati wa mchezo huo Mfaume Ali Nassor.
“Pia tumemsimamisha kocha wa Kilimani City Abrahman Mussa mpaka atuletee vyeti vyake vya ukocha na tujirizishe mana katika mchezo wao dhidi ya Black Sailors alikwenda kumzonga Muamuzi sasa tunawasi wasi mpaka na cheti chake cha ukocha”. Alisema Tedy.
Hivyo makala Azi Shaweji asimamishwa mechi nne Ligi Kuu zenj, Kocha Abrahman Mussa apigwa stop kukaa Benchi
yaani makala yote Azi Shaweji asimamishwa mechi nne Ligi Kuu zenj, Kocha Abrahman Mussa apigwa stop kukaa Benchi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Azi Shaweji asimamishwa mechi nne Ligi Kuu zenj, Kocha Abrahman Mussa apigwa stop kukaa Benchi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/azi-shaweji-asimamishwa-mechi-nne-ligi.html
0 Response to "Azi Shaweji asimamishwa mechi nne Ligi Kuu zenj, Kocha Abrahman Mussa apigwa stop kukaa Benchi"
Post a Comment