SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI

SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI
kiungo : SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI

soma pia


SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI

Sekta Binafsi imetakiwa kuwasiliana moja kwa moja na Serikali ili kutatua changamoto zinazoikabili badala ya kupitia wadau wa nje kwanza, kwa kuwa mlango wa Serikali uko wazi kwa ajili ya majadiliano na kutatua matatizo ya Sekta hiyo.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) katika Mkutano na Sekta Binafsi nchini (TPSF), Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mpango amesema kuwa ni vema Sekta Binafsi ikashirikiana na Sekta ya Umma kwa kuwa zote zinategemeana na hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na Sekta Binafsi ambayo ni imara.
“Sekta Binafsi na Sekta ya Umma hazina budi kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu, tena kwa kuaminiana kwa faida ya Sekta zote mbili na kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla” aliongeza Dkt. Mpango.
Amesema kuwa, lengo la pande zote mbili ni kuharakisha utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuongeza fursa za ajira, kipato cha mwananchi na kuondokana na umasikini uliokithiri kwa kujenga Tanzania inayoongozwa na uchumi wa Viwanda.
Dkt. Mpango alifafanua kuwa Serikali imeendelea kuyafanyia kazi mapendekezo mengi yaliyotolewa na Sekta Binafsi ikiwemo katika kuboresha mazingira ya biashara nchini ikiwemo kuondoa baadhi ya kodi zilizokuwa kero kwa wafanyabiashara.
Baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Serikali kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kumpa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Fedha mamlaka ya kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani bila kuhusisha utaratibu wa kulipa kwanza Kodi ya Ongezeko la Thamani na baadaye kuomba kurejeshewa (Refund) kwenye miradi inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo (Grants) au mikopo yenye masharti nafuu (Concessional Loans) ambayo mikataba husika ina masharti ya kutoa msamaha wa kodi hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Godfrey Simbeye akifafanua jambo kwa wafanyabiashara waliohudhuria katika Mkutano kati yao na Serikali uliolenga kujadili mafanikio na changamoto za pande hizo mbili, uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti mweza wa mkutano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akielezea kuhusu umuhimu wa majadiliano katika kutatua changamoto za kibiashara nchini, mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza na wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa kupeleka taarifa za changamoto zao Serikalini ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.


Hivyo makala SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI

yaani makala yote SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/sekta-binafsi-yatakiwa-kupeleka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI"

Post a Comment