Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni

Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni
kiungo : Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni

soma pia


Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni

WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’ jana wamemkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao Yahaya Ally Khamis, aliyeibuka na ushindi katika droo ya 15, iliyochezeshwa juzi Jumapili, huku akitokea wilayani Handeni, mkoani Tanga. 

Makabidhiano hayo yamefanyika wilayani hapa katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni, mkoani Tanga, tayari kwa kuziingiza katika matumizi ya kumkwamua kiuchumi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mchezo wao ni rahisi kucheza na kushinda, tofauti na michezo mingine inayotumia akili nyingi pamoja na uzoefu wa kufuatilia mambo mengi ya kukuletea ushindi. Alisema Biko ili mtu ashinde ni kufanya muamala kwenye simu yake ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ikiwa ni 2456, huku mchezaji akiwa haulizwi swali lolote kwenye simu yake.

“Biko hatuulizi mtu swali lolote na ndio maana zaidi ya mtu kufanya muamala ambao Sh 1,000 yake itampatia nafasi ya ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni 1,000,000 zinazolipwa kwenye simu mara baada ya kupokea ujumbe wa ushindi, huku nafasi nyingine ikiwa ni kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 ambayo Jumapili iliyopita tulimpata Khamis tuliyomkabidhi leo fedha zake.

“Tumefarijika kuja Handeni kumpatia fedha zake mshindi wetu, huku tukiwaasa Watanzania wote kujitokeza kwa wingi kucheza Biko kwa sababu ni mchezo unaotoa ushindi mzuri na haraka, hivyo chezeni kwa wingi na mara nyingi zaidi ili mjiwekee mazingira mazuri ya ushindi,” Alisema Heaven.

Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, kushoto akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 Yahaya Ally Khamis, dakika chache kabla ya kuelekea katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni walipomkabidhi pia kiasi cha fedha taslimu Sh Milioni 20 kama mshindi wa droo ya 15 ya Biko iliyochezeshwa Jumapili iliyopita. Wengine ni majirani na wadau wa Khamis, wilayani Handeni wakishuhudia wakati anakabidhiwa hundi hiyo.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wao wa Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis kulia. Makabidhiano hayo yalifanyika katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni mkoani Tanga jana. Kushoto ni afisa wa NMB, wilayani Handeni akishuhudia makabidhiano hayo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni

yaani makala yote Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/biko-yampatia-milioni-20-mshindi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni"

Post a Comment