title : UHUSIANO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI WAIMARIKA
kiungo : UHUSIANO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI WAIMARIKA
UHUSIANO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI WAIMARIKA
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wananchi na viongozi kutoka katika vijiji saba vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) ya Makao hususani Kijiji cha Makao wilayani Meatu Mkoani Simiyu, wamekiri kuwa uhusiano kati yao na Mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD, ambaye amewekeza katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA katika Kijiji cha Makao kwa ajili ya kuendeleza uhifadhi na uwindaji wa kitalii umeimarika tofauti na awali.
Hayo yalibainishwa na wananchi hao wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Enock Yakobo katika baadhi ya miradi na maeneo ya uwekezaji ya mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao.
Wamesema awali kulikuwa na mgogoro ambao ulisababisha uhusiano kati wananchi na mwekezaji kuvunjika, lakini baadaye Serikali ya Wilaya na Mkoa ziliingilia kati changamoto zote zilijadiliwa na mapungufu yote yaliyobainika yakafanyiwa kazi, ili pande zote ziweze kunufaika na uwekezaji huo.
“ Uhusiano kati ya Mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD sasa hivi uko vizuri, migogoro iliyokuwepo haipo tena, sasa hivi tunaendelea kuelimishana sisi kwa sisi, ili tusiingize mifugo kwenye eneo lilohifadhiwa kwa utalii maana linatusaidia na tunaendelea kuhamasishana kupambana na ujangili” alisema Andrea Yakobo Mkazi wa Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
“Uhusiano uko vizuri, zamani wakati kuna mgogoro tulikuwa tunashuhudia mizoga ya tembo lakini sasa hivi baada ya mwekezaji kushirikiana na wananchi kila mmoja wetu amekuwa mlinzi wa wanyama walio kwenye Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA, ajira watoto wetu wanapata kama tulivyokubaliana, wantusaidie kwenye elimu, afya na mengine” alisema Amosi Sitta kutoka Kijiji cha Makao.
Mkurugenzi wa Mwiba Holdings Ltd Bw. Abdulkadiri Mohamed akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati yaUlinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yao katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA katika Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoawa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akikagua kikosi cha kuzuia ujangili katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo (kushoto akizungumza jambo na Mkurugenzi wa MWIBA HOLDINGS LTD Bw. Abdulkadiri Mohamed wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na askari wa kikosi cha kuzuia ujangili katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala UHUSIANO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI WAIMARIKA
yaani makala yote UHUSIANO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI WAIMARIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UHUSIANO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI WAIMARIKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/uhusiano-kati-ya-mwekezaji-na-wananchi.html
0 Response to "UHUSIANO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI WAIMARIKA"
Post a Comment