title : DC ARUMERU AANZA MKAKATI MAALUM WA KUKUZA UTALII HIFADHI YA WANYAMA ARUSHA
kiungo : DC ARUMERU AANZA MKAKATI MAALUM WA KUKUZA UTALII HIFADHI YA WANYAMA ARUSHA
DC ARUMERU AANZA MKAKATI MAALUM WA KUKUZA UTALII HIFADHI YA WANYAMA ARUSHA
UTALII WETU ARUMERU
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro ameanzisha mkakati Maalum wa kukuza utalii katika Hifadhi ya wanyama ya Arusha iliyoko wilaya ya Arumeru kwa kuvitumia Vyuo vikuu na taasisi za Elimu ya Juu , Shule za sekondari binafsi na za Umma pamoja na shule za msingi na za awali zilizoko katika wilaya ya Arumeru .
Dc Muro amebuni mkakati huo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake ya kuhamasisha utalii wa ndani katika wilaya ya Arumeru ambapo safari hii ametoa maelekezo kwa wamiliki , viongozi , wakuu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu pamoja na wakuu wa shule kuweka utaratibu utakaowawezesha wanafunzi na jumuiya za watu walio kwenye taasisi zao kutembelea hifadhi ya Wanyama Arusha.
Aidha kwa kuanzia mara mbili kwa mwaka, ambapo katika zoezi la mwanzo Dc Muro amewaongoza wanafunzi , walimu na wanajumuiya ya Shule ya Haradali Winners kutembelea hifadhi ya wanyama ya Arusha ambapo miongoni mwao ni wanafunzi walioapata alama ya ufaulu ya daraja la kwanza (division one ) kutoka kila darasa na mikondo ya shule hiyo kwa gharama za Dc Muro, ambapo mwezi ujao atapeleka kundi lingine la wananfunzi wa shule ya sekondari ya Ilboru iliyoko Halmashauri ya Arusha wilaya ya Arumeru .
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akiwa na baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Haradali Winners ambao emeongozana nao kutembelea hifadhi ya wanyama ya Arusha,wakisoma maelezo kwenye vitabu vya utalii kuhusu hifadhi hiyo

Hivyo makala DC ARUMERU AANZA MKAKATI MAALUM WA KUKUZA UTALII HIFADHI YA WANYAMA ARUSHA
yaani makala yote DC ARUMERU AANZA MKAKATI MAALUM WA KUKUZA UTALII HIFADHI YA WANYAMA ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC ARUMERU AANZA MKAKATI MAALUM WA KUKUZA UTALII HIFADHI YA WANYAMA ARUSHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/dc-arumeru-aanza-mkakati-maalum-wa.html
0 Response to "DC ARUMERU AANZA MKAKATI MAALUM WA KUKUZA UTALII HIFADHI YA WANYAMA ARUSHA"
Post a Comment