WANAFUNZI 49 WAHITIMU MAFUNZO YA HOTELIA VETA JIJINI DAR

WANAFUNZI 49 WAHITIMU MAFUNZO YA HOTELIA VETA JIJINI DAR - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANAFUNZI 49 WAHITIMU MAFUNZO YA HOTELIA VETA JIJINI DAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANAFUNZI 49 WAHITIMU MAFUNZO YA HOTELIA VETA JIJINI DAR
kiungo : WANAFUNZI 49 WAHITIMU MAFUNZO YA HOTELIA VETA JIJINI DAR

soma pia


WANAFUNZI 49 WAHITIMU MAFUNZO YA HOTELIA VETA JIJINI DAR

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana amewataka maafisa maendeleo wa wilaya hiyo kuwaangalia kwa jicho la pili wanafunzi waliohitimu mafunzo VETA.

Ameyasema hayo katika mahafali ya wanafunzi 49 waliohitimu mafunzo ya Kozi ya Hotelia jana Jijini Dar es Salaam.Bwana amesema kuwa maafisa maendeleo wanatakiwa kuwaingiza wanafunzi hao katika vikundi ili wapate mikopo na kujiendeleza kiuchumi.

Amesema kuwa, wanafunzi hawa wameweza kupata mafuno hayo kupitia Kanisa la Jeshi la l wokovu na haina budi kupata fursa za mikopo kwani ni msingi mzuri kwa maendeleo yao ya baadae.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Jeshi la Wokovu Colonel Wayne Bungay amewapongeza wanafunzi hao na kuwataka waende wakajiendeleze kupitia mafunzo hayo waliyoyapata kwani wao ni tegemeo kubwa kwa maendeleo ya taifa hili.Colonel Bungay amesema, mradi huu umesaidiwa na watu wa Kanisa la Jeshi la wokovu Uholanzi, Kanisa la Jeshi la Wokovu Norway sambamba na Serikali ya Norway kuunga mkono na kusaidiana kwenye mradi huo.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha VETA Violet Fumbo amesema kuwa wanafunzi hawa wamepata mafunzo hayo na wameweza kufany vizuri na aanamini hawataufanyia mzaha na kuishia kuweka vyeti ndani.Amewataka wanafunzi hao kujiajiri na kuonyesha ujuzi wao ili jamii waweze kufahamu kuwa Chuo cha VETA kinatoa mafunzo bora na yenye weledi. 

Mbali na kukabidhiwa vyeti wanafunzi waliofanya vizuri waliweza kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke.Wanafunzi hao ni Damian Francis katika upande wa Food Production, Najat Mgaja kwa upande wa House Keeping, Hotel Management ni Turuki Mansour, Bakery ni Edna Msabi.

Mafunzo haya yatamalizika 2021, kwa jumla ya wanafunzi 300 kutoka kata 5 za Wilaya ya Temeke kuchaguliwa katika vipindi tofauti ili kuweza kusoma katika Chuo cha Veta.Wanafunzi hao wanatoka katika kata za Miburani, Chamazi, Toangoma, Makangarawe na Kilakala.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Jeshi la Wokovu Colonel Wayne Bungay akizungumza na wahitimu waliomaliza mafunzo ya Hotelia kwenye Chuo cha VETA yakiwa ndani ya mradi wa Kanisa hilo, Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeka John Bwana na Kushoto ni Rais wa vyama vya wanawake wa Jeshi la Wokovu Tanzania Colonel Deborah Bungay
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akizungumza na wahitimu na kuwapongeza kwa hatua waliyofikia ya kumaliza mafunzo ya Hotelia na kuwataka waende kujiendeleza ikiwemo na kuomba mikopo kutoka kwa Manispaa ili wajiajiri na kuacha kusubiri kuajiriwa
Mkuu wa Chuo cha VETA Violet Fumbo amewashukuru Kanisa la Jeshi la Wokovu kwa kuona na kuthamini mchango wa vijana kwenye nchi kwa kuamua kuwapatia fursa ya kupata mafunzo ndani ya Chuo chake, jumla ya wanafunzi 49 wamemaliza mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti vya VETA leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akikabidhi vyeti kwa baadhi ya wahitimu wa Kozi ya Hotelia kwenye mahafali jana Jijini Dar es Salaam, jumla ya wanafunzi 49 wamehitimu mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akikabidhi vyeti kwa baadhi ya wahitimu wa Kozi ya Hotelia kwenye mahafali   jana Jijini Dar es Salaam, jumla ya wanafunzi 49 wamehitimu mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akitoa zawadi kwa mwanafunzi bora Damian Francis wakati wa mahafali ya wahitimu wa Mafunzo ya Hotelia walio katika mradi wa Kanisa la Jeshi la wokovu wakisoma katika chuo cha VETA leo Jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja na wanafunzi waliohitimu


Hivyo makala WANAFUNZI 49 WAHITIMU MAFUNZO YA HOTELIA VETA JIJINI DAR

yaani makala yote WANAFUNZI 49 WAHITIMU MAFUNZO YA HOTELIA VETA JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI 49 WAHITIMU MAFUNZO YA HOTELIA VETA JIJINI DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/wanafunzi-49-wahitimu-mafunzo-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WANAFUNZI 49 WAHITIMU MAFUNZO YA HOTELIA VETA JIJINI DAR"

Post a Comment