title : MAKONDA AAGIZA VIPINDI VYA DINI KUFUNDISHWA MASHULENI ILI KUKUZA MAADILI NA UZALENDO
kiungo : MAKONDA AAGIZA VIPINDI VYA DINI KUFUNDISHWA MASHULENI ILI KUKUZA MAADILI NA UZALENDO
MAKONDA AAGIZA VIPINDI VYA DINI KUFUNDISHWA MASHULENI ILI KUKUZA MAADILI NA UZALENDO
* Aonya wanasiasa wanaotukana viongozi wa dini
* Moja ya barabara kupewa jina la Kardinali Pengo,heshima ya kutambua mchango wake kwa taifa.
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka maafisa elimu wa Halmashauri na Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha vipindi vya dini vinafundishwa katika shule zote ili kujenga maadili mema.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bweni, ukumbi pamoja na gari la shule katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Joseph Millenium Goba jijini Dar es salaam, Makonda amesema kuwa shule nyingi zimekuwa zikitumia muda wa vipindi vya dini kufanya mambo mengine na kusisitiza kuwa walimu wakuu wasiofuata utaratibu huo watachukuliwa hatua kali.
Aidha Makonda amewaonya wanasiasa wanaotukana viongozi wa dini kuchukua tahadhari, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayetukana kiongozi wa dini.
Amesema kuwa viongozi wa dini wamekuwa na mchango mkubwa katika kutetea uzalendo na kuhimiza maadili na amemshukuru kwa namna ya pekee Askofu Mwadhama Cardinali Polycarp Pengo Askofu wa Jimbo kuu la Dar es salaam kwa kuwa mmoja wa viongozi wazalendo kwa taifa na amehaidi moja ya barabara kubwa zinazojengwa jijini Dar es salaam zitapewa jina lake katika kutambua mchango wake na kumuenzi.
Vilevile amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwa nidhamu na sio kushinda katika mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikipotosha.Kwa upande wake Mwadhama Pengo amemshukuru Makonda kwa mchango wake na kuahidi kuiombea barabara itakayopewa jina lake pia amemshukuru Mbunge wa Hanang' Dkt. Mary Nagu kwa kuanzisha harambee ambayo imefanikisha kununua basi kwa ajili ya wanafunzi.
Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph Millenium inapatikana Goba jijini Dar es salaam na harambee ya kuchangia ujenzi huo ilianza mwaka 2016 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alichangia mifuko ya saruji na magodoro yapatayo 400 ili kuweka hali nzuri ya ujifunzaji shuleni hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (kushoto) akizindua ukumbi wa mikutano na shughuli za kitaaluma katika shule ya Mtakatifu Joseph Millenium, kulia ni Askofu Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (kulia) akiteta jambo na Askofu Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo wakati wa hafla ya uzinduzi wa bweni, ukumbi pamoja na gari la wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph Millenium, jana jijini Dar es salaam.
Viongozi wa dini na serikali wakiimba wimbo wa taifa katika hafla ya uzinduzi wa bweni, ukumbi na gari la shule ya Mtakatifu Joseph Millenium ,Goba jiji Dar es salaam.Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akifuatiwa na Askofu Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, na Mkuu wa shule hiyo Sista. Caroline Kokutekana,kushoto ni Mbunge wa jimbo la Hanang' Dkt. Mary Nagu.
Hivyo makala MAKONDA AAGIZA VIPINDI VYA DINI KUFUNDISHWA MASHULENI ILI KUKUZA MAADILI NA UZALENDO
yaani makala yote MAKONDA AAGIZA VIPINDI VYA DINI KUFUNDISHWA MASHULENI ILI KUKUZA MAADILI NA UZALENDO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA AAGIZA VIPINDI VYA DINI KUFUNDISHWA MASHULENI ILI KUKUZA MAADILI NA UZALENDO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/makonda-aagiza-vipindi-vya-dini.html
0 Response to "MAKONDA AAGIZA VIPINDI VYA DINI KUFUNDISHWA MASHULENI ILI KUKUZA MAADILI NA UZALENDO"
Post a Comment