ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI

ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI
kiungo : ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI

soma pia


ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI

NA MWAMVUA MWINYI, RUFIJI 


JUMLA ya kilo 5,623,277 za korosho zenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 16.324.9 tayari zimelipwa kwa wakulima mkoani Pwani. 

Aidha wakulima wa korosho 24,543 ,wenye kilo 14,370, 844 kati ya kilo 21,130,598 zilizopo kwenye maghala makuu wameshakikiwa, sawa na asilimia 68 . 

Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Ndikilo alitoa taarifa hiyo wakati alipokuwa akizungumza kwenye ziara yake wilaya ya Mkuranga na Rufiji.

Alisema, zoezi la uhakiki lilikuwa mwisho february 15 lakini mkoa huo unaomba kuongezewa muda hadi february 28 mwaka huu, kwakuwa umechelewa kuanza zoezi hilo na bei ya daraja la pili ilichelewa kutoka ambayo itakuwa sh. 2,640 kwa kilo .

Ndikilo alieleza, hadi tarehe 12 februari, mwaka huu jumla ya kilo 23,066,238 za korosho zimekusanywa, ambapo kilo 21,130,598, sawa na asilimia 91.6 zipo kwenye maghala makuu.

"Ghala kuu la Mwanambaya zipo kilo 6,549,204, Kibiti kilo 2,650,529, TANITA kilo 1,705,621, Kurasini PISAH kilo 3,727,669, Kurasini SCALABLE kilo 6,325,237 ,Kiegeani- Mafia kilo 213,593 na kilo 6,488,690 zipo kwenye maghala madogo ya AMCOS"alibainisha Ndikilo. 

Nae katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji, Shangwe Twamala alisema mkoa wa Pwani ulichelewa kuanza ukusanyaji wa korosho tarehe 30 Oktoba, 2018 tofauti na mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, ambayo ilianza mapema.

"Baadhi ya korosho kuendelea kuwepo kwenye maghala ya AMCOS, Ili kutatua changamoto hii, tunashauri malipo kwa wasafirishaji yafanyike kwa wakati ili waweze kufanya kazi hii"

"Kama itawezeakana tutumie magari ya jeshi kuhamisha korosho kutoka kwenye AMCOS kwenda maghala ya Kurasini"alieleza Twamala. Kwa upande wao mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga alisema, tani zaidi ya 4,000 za korosho kati ya 6,000 walizokusanya zipo chini ya sakafu ambapo wamezitandikia maturubai lakini wanahofia unyevunyevu zisije kuharibika. 

Mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Njwayo alisema, wakulima wilayani hapo wamelipwa korosho sh. bilioni 3.7 ,kwa wakulima 2,665.#


Hivyo makala ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI

yaani makala yote ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/zaidi-ya-bil-163249-zimelipwa-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI"

Post a Comment