title : UBUNGO WACHAMBUA BAJETI YAO YA FEDHA,WAJIPANGA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA JAMII
kiungo : UBUNGO WACHAMBUA BAJETI YAO YA FEDHA,WAJIPANGA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA JAMII
UBUNGO WACHAMBUA BAJETI YAO YA FEDHA,WAJIPANGA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA JAMII
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MEYA wa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam Boniface Jacob ametaja vipaumbele 11 vya halmashauri yai vilivyomo katika Bajeti ya fedha kwa mwaka 2019/2020 ambayo pamoja na mambo nengine imejikita kuboresha utoaji huduma kwa jamii kwa kuongeza fedha za kujengea Makao makuu ya Halmashauri kiasi cha Sh.millioni 700.
Pia bajeti hiyo inaonesha kuanza ujenzi wa kujenga Hospitali ya wilaya kwa kiasi cha sh.Millioni 250,pamoja na kutengwa fedha za kujenga machinjio ya kisasa kiasi cha sh.Millioni 250 pamoja fedha Sh.milioni 300 ambazo zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Mbezi( kwa ajili ya wamachinga).
Akizungumza zaidi kuhusu makadirio ya fedha hizo za bajeti jana wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam ,Meya Jacob amefanunua kuwa Serikali itatoa ruzuku ya Sh.Billioni 65.5, Sh.Millioni 750 ni michango ya Wananchi na Sh.billioni 18.4 ni makusanyo ya ndani.
Pia amesema Sh.,Billioni 72.3 ni Mishahara ya watumishi na Sh.billioni 12.3 zimeelekezwa katika miradi Mbalimbali ya Maendeleo.Aidha ameweka msisitizo kuwa Kiasi cha Sh.billioni 8.3 sawa na asilimia 60,za mapato yanayokusanywa na Halmashauri zitatumika kwa ajili ya Miradi ya maendeleo.
Jacob amezungumzia pia uimarishwaji wa Utawala bora kwa kuwatengea fedha za kiinua Mgongo ,wenyeviti wa Serikali za mitaa wanaomaliza muda wao mwaka 2019
"Kuongeza Mapato kwa kuboresha miundombinu ya ukusanyaji,kubuni vyanzo vipya,Uanzishaji wa stendi za daladala Mloganzila na Msumi,Uanzishwaji wa Masoko mapya Kiasi cha Sh.Billioni 1.7 zimetengwa
" Tumedhamiria kuongeza kiwango cha uzoaji taka Nlngumu kwa manispaa kwa kununua vifaa vya ubebaji taka kama magari na mitambo,Kiasi cha sh.billioni 3.02 kimetengwa,Ujenzi wa Mabweni ya Wavulana na Wasichana shule ya Sekondari Goba sh.Millioni 230 zimetengwa,"amesema.
Akiizungumzia zaidi bajeti hiyo amesema halmashauri itatoa mikopo kwa Vikundi vya Wanawake,Vijana na Walemavu ambapo Sh.billioni 1.38 zimetengwa. Pia kupima maeneo ya Umma,kwa kutoa hati miliki na kutwaa Maeneo ya miradi ya uwekezaji Sh.billioni 1.4 zimetengwa
Amesema bajeti hiyo itajikita pia kuboresha na kujenga niundombinu ya elimu msingi na Sekondari kwa kujenga madarasa na Nyumba za walimu, ambapo sh. billioni 1.168 zimetengwa kwa kazi hiyo.
Meya amesisitiza kuwa,Halmashauri ni chombo cha wananchi ambacho kimewekwa kisheria katika kukuza uchumi na kusogeza ajira kwa Vijana ili kupunguza Umasikini hasa wa kipato ili Kujiletea Maisha Bora.
Mkuu wa wilaya ya Ubungo,Kisare Mkori akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya hiyo waliofika katika mkutano wa baraza la Madiwani la kupitisha Bajeti ya 2019/2020 leo jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Halmashauri Manispaa ya Ubungo,Boniface Jacob (kulia) akisoma hotuba yake katika mkutano wa kupitisha bajeti ya mwa 2019-2020 leo jijini Dar es Salaam.(kushoto) Mkuu wa wilaya ya Ubungo,Kisare Mkori
Mkurugenzi wa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,Betrice (kulia) akizungumza Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya hiyo katika mkutano wa kupitisha bajeti ya Julai,2019-Juni,2020 leo jijini Dar es Salaam.
.Mkuu wa wilaya ya Ubungo,Kisare Makori (Kushoto) akiteta jambo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,Boniface Jacob wakati wa mkutano wa baraza la Madiwani la kupitisha Bajeti ya 2019/2020 leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Hivyo makala UBUNGO WACHAMBUA BAJETI YAO YA FEDHA,WAJIPANGA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA JAMII
yaani makala yote UBUNGO WACHAMBUA BAJETI YAO YA FEDHA,WAJIPANGA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA JAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UBUNGO WACHAMBUA BAJETI YAO YA FEDHA,WAJIPANGA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA JAMII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/ubungo-wachambua-bajeti-yao-ya.html
0 Response to "UBUNGO WACHAMBUA BAJETI YAO YA FEDHA,WAJIPANGA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA JAMII"
Post a Comment