title : TBC, UNESCO na EU wazindua studio ya Urithi
kiungo : TBC, UNESCO na EU wazindua studio ya Urithi
TBC, UNESCO na EU wazindua studio ya Urithi
Na Mwandishi wetu
SHIRIKA la Utangazaji Nchini (TBC) limezindua studio kubwa ya Kumbukumbu ya ukombozi wa Afrika ya Mwalimu Nyerere katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam.
Studio hiyo yenye kuhifadhi historia ya kumbukumbu ya ukombozi barani Afrika zilizopo katika kanda za sauti na video imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya TBC na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na wadau wengine wa maendeleo.
Kuwapo kwa studio hiyo kumelenga kuongeza uwajibikaji, uwezo wa kupata taarifa za zamani na kuongeza uratibu wa menejimenti ya hifadhi ya mambo muhimu ambayo ni ya urithi wa Tanzania.
Studio hiyo ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa hifadhi ya mambo ya urithi (TAHAP) wenye lengo la kuhamasisha hifadhi na utunzaji wa urithi wa Tanzania na kumbukumbu za mapambano ya ukombozi katika bara la Afrika, pia itaongeza uelewa wa watanzania juu ya urithi wao ambao umekuwa ukiongezeka jinsi miaka inavyozidi kusonga mbele.
Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo na Msemaji Mkuu wa serikali Dk. Hassan Abbas alisema kwamba serikali itaendelea kuhakikisha kwamba urithi wa nchi hii unahifadhiwa kwa manufaa ya kizazi kijacho.
"Kwa sasa tunaondoka katika mfumo wa maandiko, sauti na video. Sisi kama serikali tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba matukio yetu ya kihistoria yanarekodiwa na kuhifadhiwa vyema. Hatua hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa historia kwa watu wetu na serikali kwa ujumla," alisema Dk Abbas .
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ,Dkt. Hassan Abbas (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Ms.Anna Therese Ndong-Jatta(kulia) wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba, Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw. Charlie Stuart na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas (wapili kulia) akishuhudia Mkurugenzi Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. Anna Therese Ndong-Jatta (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba moja ya Kamera pamoja na vifaa mbalilmbali vya utangazaji vilivyotolewa msaada na UNESCO kwa kushirikiana na wadua na Washirika wa Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini. Kushoto ni Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bi. Charlie Stuart.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas (wa pili kulia) akishuhudia Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bi. Charlie Stuart akimkabidhi moja ya kifaa cha kurekodia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba kati ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa msaada na UNESCO kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas (katikati) akishuhudia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez akimkabidhi moja ya kifaa cha kuhifadhia kumbukumbu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba kati ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa msaada na UNESCO kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
Kutoka Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw.Charlie Stuart, Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi.Anna Therese Ndong-Jatta, ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya utangazaji vilivyotolewa msaada na UNESCO Kwa kushirikiana na wadau wa mradi wa Umoja wa Ulaya.(EU)
Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. Anna Therese Ndong-Jatta, (wa tatu kulia) Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw. Charlie Stuart (kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba, wakimsikilza kwa makini mmoja wa wafanyakazi wa TBC akiwaonyesha moja ya mitambo iliyotumika kurekodia enzi kupigania ukombozi wa Afrika.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TBC, UNESCO na EU wazindua studio ya Urithi
yaani makala yote TBC, UNESCO na EU wazindua studio ya Urithi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TBC, UNESCO na EU wazindua studio ya Urithi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tbc-unesco-na-eu-wazindua-studio-ya.html
0 Response to "TBC, UNESCO na EU wazindua studio ya Urithi"
Post a Comment