title : YANGA WAKUBALI KICHAPO TAIFA DHIDI YA GOR MAHIA
kiungo : YANGA WAKUBALI KICHAPO TAIFA DHIDI YA GOR MAHIA
YANGA WAKUBALI KICHAPO TAIFA DHIDI YA GOR MAHIA
Baada ya kuambulia kichapo cha mabao 3-2 jana katika mchezo wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kkikosi cha Yanga kimeweka rekodi ya kucheza dakika 360 bila kupata alama tatu.
Yanga imepoteza mechi hiyo ya mkondo wa pili kwa mabao yaliyofungwa kimiani na George Odhiambo, Jacques Tuyisenge na Haron Shakava kwa upande wa Gor Mahia.
Kwa upande wa Yanga, mabao yamefungwa na kiungo mshambuliaji Deus Kaseke ambaye alisajiliwa kutoka Singida United pamoja na Raphael Daudi.
Yanga imeshindwa kupata alama hizo kutokana na kupata suluhu moja pekee kunako kundi D dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na ikipoteza mechi mbili ilizofungwa na Gor Mahia pamoja na moja dhidi ya MC Alger.
Yanga imeshikilia mkia ikiwa na alama 1 ambayo iliipata baada ya matokeo ya 0-0 katik amchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Rayon na kujiweka katika nafasi ya 4.
Baada ya mechi hiyo, msimamo sasa unaonesha timu zote zimecheza mechi 4 huku MC Alger ikiwa kileleni na alama 8 ikiizidi Gor Mahia kwa tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga huku Rayon ikishika namba tatu na Yanga ikiwa mwishoni
Hivyo makala YANGA WAKUBALI KICHAPO TAIFA DHIDI YA GOR MAHIA
yaani makala yote YANGA WAKUBALI KICHAPO TAIFA DHIDI YA GOR MAHIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala YANGA WAKUBALI KICHAPO TAIFA DHIDI YA GOR MAHIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/yanga-wakubali-kichapo-taifa-dhidi-ya.html
0 Response to "YANGA WAKUBALI KICHAPO TAIFA DHIDI YA GOR MAHIA"
Post a Comment