title : MWAKINYO, ZARIKA WAJIFUA UINGEREZA KUELEKEA PAMBANO LA MACHI 23.
kiungo : MWAKINYO, ZARIKA WAJIFUA UINGEREZA KUELEKEA PAMBANO LA MACHI 23.
MWAKINYO, ZARIKA WAJIFUA UINGEREZA KUELEKEA PAMBANO LA MACHI 23.
Bondia namba moja wa uzito wa Super Welterweight, Hassan Mwakinyo na bondia nyota wa kike nchini Kenya, Fatuma Zarika wamewasili mjini Liverpool kujiandaa na pambano la ngumi za kulipwa mjini Nairobi, Kenya mwezi ujao.
Mwakinyo na Zarika ambapo wapo chini ya udhamini wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa, watapambana na mabondia tofauti katika pambano lililopewa jina la Nairobi Fight Night katika ukumbi ambao utatangazwa hapo baadaye.
Mwakinyo ambaye bondia namba 16 kati ya mabondia 1,842 kwa mujibu wa viwango vya mtandao maarufu wa ngumi za kulipwa Duniani, Boxrec, Bondia huyo mzawa wa mkoa wa Tanga, kwa sasa ana rekodi ya kushinda mapambano 24, kati ya hayo, 10 kwa knockout (KO) na kupoteza mawaili ikiwa moja kwa KO.
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema kuwa mabondia hao wawili watakuwa chini ya kocha wa bondia nyota, Tony Bellew ambaye alimchapa kwa TKO mara mbili, bondia maarufu, David Haye.
Abbas alisema kuwa Mwakinyo na Zarika watarejea moja kwa moja nchini Kenya Machi 16 tayari kwa mapambano yao. Zarika ambaye ni maarufu kwa jina la “Irone Fist” atatetea ubingwa wake wa Baraza la Ngumi za Kulipwa (WBC) wa uzito wa Super Bantamweight, atapambana na bondia nyota kutoka Zambia, Catherine Phiri.

Abbas aliwaomba mashabiki wa ngumi za kulipwa kufika kwa wingi wakati wa mapambano hayo ili kuwapa hamasa mabondia hao ambao ni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wake, Mwakinyo aliishukuru kampuni ya SportPesa kwa kuwatafutia kambi ya mazoezi, jambo ambalo hakuwa anafanya kabla ya kupata umaarufu.
“Ni faraja kwangu na mchezo wa ngumi za kulipwa pia. Naamini mabondia wengine wataongeza bidii ili kuweza kufikia kiwango change na kupata wadhamini kama SportPesa ambao wamenyesha njia kwangu,” alisema Mwakinyo.
Hivyo makala MWAKINYO, ZARIKA WAJIFUA UINGEREZA KUELEKEA PAMBANO LA MACHI 23.
yaani makala yote MWAKINYO, ZARIKA WAJIFUA UINGEREZA KUELEKEA PAMBANO LA MACHI 23. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWAKINYO, ZARIKA WAJIFUA UINGEREZA KUELEKEA PAMBANO LA MACHI 23. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mwakinyo-zarika-wajifua-uingereza.html
0 Response to "MWAKINYO, ZARIKA WAJIFUA UINGEREZA KUELEKEA PAMBANO LA MACHI 23."
Post a Comment