WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI KUWAKAMATA WAENDESHA BODABODA WAKIWA HAWAJAVAA SARE

WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI KUWAKAMATA WAENDESHA BODABODA WAKIWA HAWAJAVAA SARE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI KUWAKAMATA WAENDESHA BODABODA WAKIWA HAWAJAVAA SARE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI KUWAKAMATA WAENDESHA BODABODA WAKIWA HAWAJAVAA SARE
kiungo : WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI KUWAKAMATA WAENDESHA BODABODA WAKIWA HAWAJAVAA SARE

soma pia


WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI KUWAKAMATA WAENDESHA BODABODA WAKIWA HAWAJAVAA SARE

Na Felix Mwagara, MOHA-Bukoba.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari Polisi nchini kukamata pikipiki wakiwa hawana sare za Jeshi.

Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa uhuru, Mayunga, mjini Bukoba Mkoani Kagera, leo, Lugola alisema polisi wanapaswa kufuata utaratibu wa kijeshi hasa wanapokamata vyombo vya moto na siyo kuvunja utaratibu.

Lugola aliongeza kuwa, bodaboda zinazovunja sheria za usalama barabarani zinapaswa kukamatwa bila kuwaonea huruma, ila ni kosa Polisi kuwanyanyasa vijana hao ambao wanapata ridhiki kupitia biasahara hiyo. “Mnapaswa kukamata hizi bodaboda zinapofanya makosa, tabia ya kukurupuka huku mkitafuta fedha zisizo halali, huko ni kuwaonea waendesha bodaboda,” alisema Lugola.

Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda mjini Bukoba na Tanzania kwa ujumla wafuate sharia za usalama barabarani zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa. Lugola ameanza ziara yake ya siku nane mkoani humo akitembelea Wilaya zote za Mkoa huo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.







Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na mamia ya wananchi mjini Bukoba Mkoani Kagera, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Mayunga mjini humo, leo. Lugola licha ya kuwa amewataka waendesha bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani, lakini ametoa onyo kwa Polisi mjini humo kuacha kuwakamata waendesha bodaboda wakiwa hawajavaa sare. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Mkazi wa mjini Bukoba alipokuwa anaeleza kero yake mara baada ya Waziri huyo kuwaita wananchi hao mbele waweze kutoa kero zao, mara baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Mayunga mjini humo, leo. Lugola licha ya kuwa amewataka waendesha bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani, lakini ametoa onyo kwa Polisi mjini humo kuacha kuwakamata waendesha bodaboda wakiwa hawajavaa sare. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsalimia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Bashiru Ally, wakati alipoonana naye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, leo. Lugola yupo Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi akitembelea Wilaya zote, akisikiliza kero mbalimbali za watumishi wa Wizara yake pamoja na wananchi mkoani humo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akitoka Kituo Kikuu cha Polisi cha mjini Bukoba mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Kituo hicho, leo, kwa kufuatilia utendaji kazi wao. Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoani humo, ACP Raymond Mwampashe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 



Hivyo makala WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI KUWAKAMATA WAENDESHA BODABODA WAKIWA HAWAJAVAA SARE

yaani makala yote WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI KUWAKAMATA WAENDESHA BODABODA WAKIWA HAWAJAVAA SARE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI KUWAKAMATA WAENDESHA BODABODA WAKIWA HAWAJAVAA SARE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/waziri-lugola-apiga-marufuku-polisi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI KUWAKAMATA WAENDESHA BODABODA WAKIWA HAWAJAVAA SARE"

Post a Comment