title : NISHATI WAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS KUWEZESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO
kiungo : NISHATI WAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS KUWEZESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO
NISHATI WAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS KUWEZESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO
Na Veronica Simba – Geita
Wizara ya Nishati inatekeleza mkakati wa kuwaunganishia umeme wa uhakika wachimbaji wadogo wa madini kote nchini, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais John Magufulu kuiwezesha sekta hiyo izalishe kwa tija kwa manufaa yao binafsi na ya Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu, kinachomilikiwa na kampuni ya Padalu, kijijini Lumasa, Chato; Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa eneo hilo, Dkt Medard Kalemani, alisema serikali imefunga transfoma tano zenye uwezo wa KVA 400 hadi 1,000 ili kuwawezesha wachimbaji wadogo wa Geita kuzalisha kwa tija.
“Umeme huu mkubwa utawawezesha wachimbaji kuchimba , kuchenjua na kuongeza thamani dhahabu yao ili kuiongezea thamani, iwapatie faida na waweze kulipa kodi na mrabaha serikalini,” alisema.
Akieleza zaidi, Waziri Kalemani alisema yako maeneo mkoani humo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo lakini akabainisha kuwa utaratibu wa kufunga transfoma nyingine tano zenye uwezo uleule, unafanyika ili kuyafikia maeneo ya wachimbaji yaliyosalia ikiwemo Mbogwe na Nyakafuru.
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (kushoto) na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia), wakifungua kitambaa maalum kilichofunika jiwe la msingi la kiwanda cha uchenjuaji dhahabu cha Padalu, kilichopo Chato Geita, kuashiria uzinduzi rasmi. Hafla hiyo ilifanyika Januari 2, 2019.
Msimamizi wa Kiwanda cha kuchakata dhahabu cha Padalu, kilichopo Chato Geita, Abel Lucas (kulia), akitoa maelezo jinsi kinavyofanya kazi kwa Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani pamoja na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, na ujumbe waliofuatana nao, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda hicho, Januari 2, 2019.
Msimamizi wa Kiwanda cha kuchakata dhahabu cha Padalu, kilichopo Chato Geita, Abel Lucas (kushoto), akitoa maelezo jinsi kinavyofanya kazi kwa Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili – kulia), wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda hicho, Januari 2, 2019.
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (katikati), akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto), walipowasili kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Padalu kilichopo Chato Geita, Januari 2, 2019. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Msafiri Mtemi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Padalu kilichopo jimboni mwake, Chato Geita, Januari 2, 2019.
Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Padalu kilichopo jimboni humo, Chato Geita, Januari 2, 2019.
Hivyo makala NISHATI WAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS KUWEZESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO
yaani makala yote NISHATI WAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS KUWEZESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NISHATI WAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS KUWEZESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/nishati-waunga-mkono-jitihada-za-rais.html
0 Response to "NISHATI WAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS KUWEZESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO"
Post a Comment