title : KIGOGO MWINGINE BENKI I&M AUNGANISHWA KESI YA MFANYABIASHARA ALIYETAJWA NA RAIS DKT MAGUFULI
kiungo : KIGOGO MWINGINE BENKI I&M AUNGANISHWA KESI YA MFANYABIASHARA ALIYETAJWA NA RAIS DKT MAGUFULI
KIGOGO MWINGINE BENKI I&M AUNGANISHWA KESI YA MFANYABIASHARA ALIYETAJWA NA RAIS DKT MAGUFULI
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii.
Meneja wa benki ya I&M tawi la Kariakoo, Sameer Khan, amefikishwa Katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuunganishwa na
mfanyabiashara maarufu aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takribani Sh. Milioni Saba kwa dakika, Mohamed Yusufali na mfanyakazi wake Arital Maliwala ambapo wote wamesomewa mashtaka mapya 506.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mapema Leo asubuhi washtakiwa Yusufali na Maliwata kufutiwa mashtaka yao ya zamani mbele ya Hakimu Mkazi Janet Mtega chini ya kifungu cha sheria cha 91(1) cha Mwenendo wa makosa ya jinai ambapo upande wa mashtaka waliomba kuliondoa shtaka hilo kwa sababu DPP hana nia Ya kuendelea na mashtaka dhidi yao. Haya hivyo Washtakiwa walikamatwa tena.
Awali, Yusufali na Maliwala. Walikuwa wakikabiliwa na jumla ya mashtaka 601 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 14
Akisoma hati ya mashtaka mapya wakili wa serikali Mwandamizi Patrick Mwita, akisaidiana na Ester Martin na Wakili kutoka Takukuru Leornad Swai wamewasomea washtakiwa mashtaka 506, ambapo wanakabiliwa na mashtaka ya 293 Ya kughusi, mashtaka 132 Ya kutoa taarifa za uongo na shtaka moja La kwepa kodi Ya zaidi ya Sh. BIL. 24
Pia mshtakikwa Khan anakabiliwa na mashtaka 12 ya utakatishaji huku Yusufali na Maliwata wakikabiliwa na mashtaka 50 ya utakatishaji. Shtaka jingine dhidi ya washtakiwa wote ni kula njama ya kutenda kosa la kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 24.
Katika shtaka la kuisababishia serikali hasara imedaiwa, katika tarehe tofauti tofauti, kati ya Januari 2008 na Januari 2016 washtakiwa waliwasilisha nyaraka za uongo huko Katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh. 24.303.777.4260.70.
Haya hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi Mahakama Kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wako kwenye hatua za mwisho kufaili kesi Mahakama Kuu Kitengo cha mafisadi.
Kesi hiyo itatajwa tena Mahakamani hapo Februari 18.2019
Meneja wa benki ya I&M tawi la Kariakoo, Sameer Khan akifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuunganishwa namfanyabiashara maarufu aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takribani Sh. Milioni Saba kwa dakika, Mohamed Yusufali na mfanyakazi wake Arital Maliwala ambapo wote wamesomewa mashtaka mapya 506.
Hivyo makala KIGOGO MWINGINE BENKI I&M AUNGANISHWA KESI YA MFANYABIASHARA ALIYETAJWA NA RAIS DKT MAGUFULI
yaani makala yote KIGOGO MWINGINE BENKI I&M AUNGANISHWA KESI YA MFANYABIASHARA ALIYETAJWA NA RAIS DKT MAGUFULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIGOGO MWINGINE BENKI I&M AUNGANISHWA KESI YA MFANYABIASHARA ALIYETAJWA NA RAIS DKT MAGUFULI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/kigogo-mwingine-benki-i-aunganishwa.html
0 Response to "KIGOGO MWINGINE BENKI I&M AUNGANISHWA KESI YA MFANYABIASHARA ALIYETAJWA NA RAIS DKT MAGUFULI"
Post a Comment