title : CHAMA CHA WASANII WA KIZAZI KIPYA ZANZIBAR KUZINDUA TAMASHA LA WAZI
kiungo : CHAMA CHA WASANII WA KIZAZI KIPYA ZANZIBAR KUZINDUA TAMASHA LA WAZI
CHAMA CHA WASANII WA KIZAZI KIPYA ZANZIBAR KUZINDUA TAMASHA LA WAZI
CHAMA Cha wasanii wa Kizazi kipya Zanzibar (ZFU) , kimeandaa tamasha la Muziki Safari ya Mapinduzi ambalo linatarajiwa kufanyika Desemba 15 mwaka huu kwa lengo la kuenzi fikra za Mapinduzi na kutangaza kazi mbali mbali zinazofanywa na Wasanii wa kizazi kipya nchini.
Akizungumza mapema leo mjini Unguja na waandishi wa habari Rais wa Chama hicho,Mohamed Abdallah 'Laki wa Promise' amesema Chama hicho kimeamua kufanya tamasha hilo ambalo litafanyika katika jimbo la Mpendae Uwanja wa Zantex litasaidia kukumbusha jamii umuhimu wa fikra za mapinduzi.
Rais huyo amesema katika tamasha hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Unguja, Abdulrahman Khatib ambapo kabla ya kuanza kwa tamasha hilo kutatanguliwa na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, uvutaji kamba na kukimbiza kuku. "Lengo kubwa ni kuchochea fikra za mapinduzi zilizofanywa na wanamapinduzi ambao wamepoteza maisha yao kwa ajili yetu ambapo kwa sasa tunaona mafanikio yake ikiwemo kuwepo kwa amani mpaka sasa hivyo ni jambo la kuwakumbusha Wanzanzibari.
kwa hiyo tutatumia vipaji vyetu vya kuimba kuwaambia jamii,"amesema Laki kuwa ni jukumu la Chama hicho kupitia sanaa kuwahabarisha jamii umuhimu wa mapinduzi ya Januari 12, mwaka 1964 na kwamba lazima yalindwe kwa njia yeyote ile na kwamba kupitia tamasha hilo litasaidia kuipa jamii hisia kali za Mapinduzi hayo. "Tamasha hili litaanza kuanzia saa 6 mchana hadi saa 12 jioni hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi na kwamba wasanii wengi watatoka Unguja na Pemba katika kutuimbuiza tamasha hilo na katika michezo itakayochezwa washindi watapewa zawadi mbalimbali,"ameeleza Rais huyo.
RAIS wa Chama Cha Wasanii Zanzibar Mohamed Abdalla 'Laki wa Promise' (wa pili kushoto), Msemaji wa Chama hicho Rashid Mustaafa 'Spaider'(wa kwanza kushoto),Mwenyekiti wa Tamasha Salum Said(wa kwanza kulia) wakizungumza na waandishi wa habari juu ya ufunguzi wa tamasha hilo.
BAADHI ya Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Habari mbali mbali visiwani Zanzibar wakisikiliza maelezo ya Rais wa Chama Cha Wasanii Zanzibar Mohamed Abdallah 'Laki wa Promise' juu ya uzinduzi wa Tamasha la muziki Safari ya Mapinduzi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala CHAMA CHA WASANII WA KIZAZI KIPYA ZANZIBAR KUZINDUA TAMASHA LA WAZI
yaani makala yote CHAMA CHA WASANII WA KIZAZI KIPYA ZANZIBAR KUZINDUA TAMASHA LA WAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHAMA CHA WASANII WA KIZAZI KIPYA ZANZIBAR KUZINDUA TAMASHA LA WAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/chama-cha-wasanii-wa-kizazi-kipya.html
0 Response to "CHAMA CHA WASANII WA KIZAZI KIPYA ZANZIBAR KUZINDUA TAMASHA LA WAZI"
Post a Comment