title : TANZANIA YAFUNGUA OFISI NDOGO YA UBALOZI HONGKONG CHINA
kiungo : TANZANIA YAFUNGUA OFISI NDOGO YA UBALOZI HONGKONG CHINA
TANZANIA YAFUNGUA OFISI NDOGO YA UBALOZI HONGKONG CHINA
Na Grace Semfuko-MAELEZO
Tanzania imefungua ofisi ndogo ya kibalozi Hongkong nchini China ambayo itahudumia masuala ya kidiplomasia na kuongozwa na Balozi wa Heshima wa Tanzania Dkt Annie Wu alieteuliwa Septemba 2 mwaka huu na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga wakati alipohudhuria mkutano wa wa mahusiano ya China na Afrika, FOCAC huko Beijing nchini China.
Ofisi hiyo mpya katika jiji la Hongkong, nchini China itasimamia masuala ya kibalozi na kuwasogezea karibu huduma hizo, tofauti na hapo awali ambapo huduma za kibalozi zilikuwa zikipatikana Beijing.
Akizungumza Jijini Hongkong nchini China jana, Balozi wa Tanzania nchini humo, Mbelwa Kairuki, alisema ni fursa kwa watanzania na wachina kutumia ofisi ya Hongkong kupata huduma mbalimbali katika ofisi hiyo kwa urahisi.
Kwa upande wake Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini China, Dkt. Annie Wu ameonyesha kufurahishwa kuaminiwa na Serikali ya Tanzania kwa majukumu hayo ya heshima aliyopewa na kuihakikishia serikali kuwa pamoja na mambo ya kidiplomasia, ataitangaza Tanzania kwa wawekezaji ili kuvutia uwekezaji zaidi.
Aidha amewakaribisha wadau wote watembelee ofisi mpya ya Tanzania ili kupata taarifa husika kuhusu utalii, biashara na uwekezaji kwa manufaa ya Tanzania na China.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TANZANIA YAFUNGUA OFISI NDOGO YA UBALOZI HONGKONG CHINA
yaani makala yote TANZANIA YAFUNGUA OFISI NDOGO YA UBALOZI HONGKONG CHINA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YAFUNGUA OFISI NDOGO YA UBALOZI HONGKONG CHINA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/tanzania-yafungua-ofisi-ndogo-ya.html
0 Response to "TANZANIA YAFUNGUA OFISI NDOGO YA UBALOZI HONGKONG CHINA"
Post a Comment