title : MWENYEKITI UWT ILALA: UKIDONDOKA KIBIASHARA USIKATE TAAMAA ONAHAWA.
kiungo : MWENYEKITI UWT ILALA: UKIDONDOKA KIBIASHARA USIKATE TAAMAA ONAHAWA.
MWENYEKITI UWT ILALA: UKIDONDOKA KIBIASHARA USIKATE TAAMAA ONAHAWA.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake CCM (UWT) Wilayani Ilala, Amina Dodi ,amewataka wanawake Wilayani Ilala kutokata tamaa katika ujasiliamali kutokana na changamoto wanazo pitia bali ziwaimarishe kwa kuwaongezea uzoefu nakufikiri zaidi kuzikifursa za kiuchumi.
Dodi , ametoa usahauri huo katika semina ya Ujasiliamali ya kufunga mwaka 2018 na kuukaribisha mwakampya 2019 , ambapo amesema kuwa umoja huo upo imara na umeendelea kupata wanachama wapya kila siku kutokana na kazi nzuri zinazo fanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kusema kuwa wanawake wa Ilala wataendelea kumuunga mkono kwa kufanya kazi .
“Ninyi akina Mama mnafikilia kupatatu ,(kuwini ) maisha nipamoja na kupata elimu, naomba niwatake tuwe watu wa wasomaji wa habari mbalimbali ,hata Trump wa Marekani ,alidondoka kibiashara akaja akainuka baadaye ,tuangalie Reginard Mengi alikuwa na Gazeti Alasiri akadondoka lakini hakukata tama,na kwenye uujasiliamali hutakiwi kukata tama wala usije ukalalamika sana kwamba mimi mbona nafanya kazi nadondoka uwe makini tu nabiasharayako ukidondoka utanyanukatu naomba wamama niwatie nguvu mwaka huu 2019 utakuwa na mafanikio”Alisema.
Amesema ,mwaka uliopita ulikuwa na mafanikio mengi kwa upande wa (UWT ) Ilala na kwamba wameweza kutimiza malengo yao mengi ikiwemo kupata hati ya kiwanja chao ambacho wanakitafutia wawekezaji ili kuongeza kipato cha umoja,na pia wameweza kuimarisha chama na umoja ,na wamepata semina zakutosha kuhusu ujasiliamali na sasa wanaweza kuendesha siasana uchumi.
“Uchumi na saiasa vinakwenda sawa wanawake hawa tumewajengea uwezo wa kujiimarisha kiuchumi na wanaweza kufanya siasa safi ,unaweza kuwa na siasa lakini uchumi ukilegalega huwezi kufanikiwa, kwahiyo kwaniaba ya wanawake (UWT ) Ilala tunamshukuru Rais kwa kujenga uchumi na tunamuombea Mungu ampe Afyanjema iliaweze kutekeleza mambo mengine mwaka huu 2019.
Katika semina hiyo wanawake hao wamefundishwa mambo mbalimbali ikiwemo elimu juu ya Mikopo, namna ya kuandika katiba ya vikundi ,na namna ya kubuni na kuanzisha biashara,Asha Johari ni katibu UWT kata ya Gerezani yeye ameishukuru UWT ,Manispaa ya Ilala na serikali kwa kutoa mikopo isiyo na riba ambayo imekuwa ukombozi kwa akinamama ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo wanawake waliteseka kwa kutozwa riba kubwa.
“Tulikuwa tunapata mikopo kutoka kwa mabenk ambayo ilikuwa nariba kubwa ya asilimia kumi hadi kumi natano ya mkopo sasa tunafaidika na huu usio na riba na tunajivuni serikalli hii inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi, imemwokoa mwanamke kwa kiasi kikubwa “Alisema
Moja ya mambo ambayo yamerudisha nyuma vikundi vingi nikuwa na katiba zisizo faa ,ambapo katika semina hiyo yametolewa mafunzo ya kuandika katiba ,Ktiba ni muhimu sana na kilakikundi kinahitaji Katiba kutokana na kutokuwa na ujuzi huu wa kuandika katiba vikundi vingi vimekwama kupewa mikopo kutokana na kukopi Ktiba za vikundi vingine .
“Kwamafunzo haya majukumu yetu sasa kama viongozi ni kwenda chini kwa kuwafundisha wanawake na hata vijana ambao hawana mafunzo haya nao tuta wasaidia ii wapate katiba bora ‘’Alisema Aziat Salim Juma Katibu UWT kata ya Buyuni.
Pamoja na hayo katika semina hiyo wanawake wameweza kujifunza ni uthubutu wa kuanzisha biashara , kujiamini na kuwa na mtazamo wa mbele zaidi kibiashara na wamemshukuru Mwenyekiti kwa kuwapatia mkufunzi kutoka Uingereza ambaye pia amewaahidi kuwa yatfutia masoko ya bidhaa zao .
“Ninachoweza kuwashauri wanawake wajasiliamali wenzangu ni kuviweka vituvyetu katika hali ya usafi zaidi viewe vya kisasa vinavyoweza kuuzika hadi masoko ya nje nami nitashuka huko chini katika matawi kuwaelekeza ili waweze kuzingatia haya “ Alisema Magreth Cheka katibu UWT kata ya Kipawa.
Hivyo makala MWENYEKITI UWT ILALA: UKIDONDOKA KIBIASHARA USIKATE TAAMAA ONAHAWA.
yaani makala yote MWENYEKITI UWT ILALA: UKIDONDOKA KIBIASHARA USIKATE TAAMAA ONAHAWA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWENYEKITI UWT ILALA: UKIDONDOKA KIBIASHARA USIKATE TAAMAA ONAHAWA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mwenyekiti-uwt-ilala-ukidondoka.html
0 Response to "MWENYEKITI UWT ILALA: UKIDONDOKA KIBIASHARA USIKATE TAAMAA ONAHAWA."
Post a Comment