title : WAKAZI DISUNYARA WATUMIA SH. 4,000 KUFUATA VIPIMO IKIWEMO CHA MALARIA UMBALI WA KM. 10 KWENDA NA KURUDI
kiungo : WAKAZI DISUNYARA WATUMIA SH. 4,000 KUFUATA VIPIMO IKIWEMO CHA MALARIA UMBALI WA KM. 10 KWENDA NA KURUDI
WAKAZI DISUNYARA WATUMIA SH. 4,000 KUFUATA VIPIMO IKIWEMO CHA MALARIA UMBALI WA KM. 10 KWENDA NA KURUDI
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA VIJIJINI
ZAHANATI ya Disunyara, kata ya Kilangalanga Kibaha Vijijini, inakabiliwa na ukosefu wa maabara hali inayosababisha kufuata vipimo ikiwemo cha malaria na damu kituo cha afya Mlandizi ambako kuna umbali wa km kumi kwenda na kurudi na nauli ya pikipiki sh. 4,000.
Kutokana na hali hiyo wakazi wa eneo hilo wamejitolea kuanza ujenzi wa maabara ambapo mbunge wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu amechangia mifuko 30 ya saruji .
Akichangia mifuko hiyo,alisema vipimo ni suala muhimu ambalo inahitajika nguvu ya pamoja kumaliza ujenzi huo. “Baada ya kusikia wananchi wameanza juhudi hizo ndipo nilipoguswa kuwaunga mkono ili kuendelea na ujenzi,alielezea Subira.
Nae diwani wa kata hiyo, Mwajuma Denge alisema wananchi wanapata shida kufuata huduma ya vipimo umbali mrefu. Aliwaomba wadau kuendelea kujitokeza kuchangia ili kumaliza ujenzi huo waweze kupata japo vipimo vya awali karibu. Kwa upande wake mganga mfawidhi wa zahanati ya Disunyara ,Maimuna Yusuph alitaja tatizo la ukosefu wa chumba cha maabara kunasababisha akinamama wajawazito kwenda Mlandizi kufuata vipimo na wakati mwingine hushindwa kutokana na ukosefu wa nauli.
Tatizo jingine ni vitanda vya kuzalia kwani kilichopo ni kimoja, kingine kibovu hivyo mahitaji ni vitanda vingine viwili ili kukidhi mahitaji. Mkazi wa Disunyara Mwajuma Juma alimshukuru Subira kwa kuwashika mkono ili kumkomboa mwanamke. Alisema endapo maabara hiyo ikikamilika itasaidia wakazi wenye mahitaji ya vipimo hasa akinamama na watoto.

Mbunge viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu akizungumza wakati alipokwenda kutembelea zahanati ya Disunyara, huko Kibaha Vijijini. (picha na Mwamvua Mwinyi) .
Hivyo makala WAKAZI DISUNYARA WATUMIA SH. 4,000 KUFUATA VIPIMO IKIWEMO CHA MALARIA UMBALI WA KM. 10 KWENDA NA KURUDI
yaani makala yote WAKAZI DISUNYARA WATUMIA SH. 4,000 KUFUATA VIPIMO IKIWEMO CHA MALARIA UMBALI WA KM. 10 KWENDA NA KURUDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI DISUNYARA WATUMIA SH. 4,000 KUFUATA VIPIMO IKIWEMO CHA MALARIA UMBALI WA KM. 10 KWENDA NA KURUDI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/wakazi-disunyara-watumia-sh-4000.html
0 Response to "WAKAZI DISUNYARA WATUMIA SH. 4,000 KUFUATA VIPIMO IKIWEMO CHA MALARIA UMBALI WA KM. 10 KWENDA NA KURUDI"
Post a Comment