TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII

TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII
kiungo : TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII

soma pia


TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII


MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha shughuli mbali mbali za jamii, kwa kutoa misaada yenye tija.

Hilo limekuwa bayana leo tarehe 12 Disemba, 2018 kwenye Kijiji cha Makumbosho Jijini Dar es Salaam, ambapo TAA imetoa msaada wa fulana 100 kwa ajili ya kufanikisha Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba, 2018 katika Uwanja wa Mazaina Chato.

Akizungumza katika Mkutano wa waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TAA, Bw. Abdi Mkwizu amesema Mamlaka ina wajibu mkubwa wa kuunga mkono shughuli za kijamii, kwa kutoa misaada ya mbalimbali.

“Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ina wajibu wa Kusimamia, kuendesha, kuboresha na kuendeleza Viwanja vya Ndege Tanzania lakini pia mbali na kutoa huduma hizo tuna wajibu wa kushiriki katika shughuli za kijamii, kwa wadau ambao wanatufanya sisi tuwepo,” amesema Bw. Mkwizu.

Pia Bw. Mkwizu amebainisha kwamba TAA inahudumia Viwanja 58 vilivyopo Tanzania Bara chini ya serikali, hivyo ni wajibu wao kushiriki katika shughuli za kusaidia jamii sehemu yeyote ile kulingana na uhitaji na bajeti iliyopo.
Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga akizungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajia kufanyika Disemba 22, 2018. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Abdi Mkwizu (kulia) na Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi G;unze (kushoto). Mkutano huo wa waandishi wa habari umefanyika leo katika Kijiji cha Makumbusho. 
Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze (kushoto), Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia) kwa pamoja wakionesha tangazo la tamasha la Utamaduni la Chato lenye kauli mbiu ya “Maendeleo ya Viwanda yasiache Utamaduni nyuma”. Tukio hilo limefanyika leo kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari katika Kijiji cha Makumbusho. 
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia), akikabidhi moja ya fulana 100 zilizotolewa na TAA kwa muandaaji wa Tamasha la Utamaduni la Chato, Bw. Amon Mkoga (kushoto), Katikati anayeshughudia ni Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze. Tamasha hilo litafanyika Disemba 22, 2018. 



Hivyo makala TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII

yaani makala yote TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/taa-yaendelea-kutoa-kwa-jamii.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII"

Post a Comment