title : RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA AL NAKHIL YA DUBAI IKULU ZANZIBAR
kiungo : RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA AL NAKHIL YA DUBAI IKULU ZANZIBAR
RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA AL NAKHIL YA DUBAI IKULU ZANZIBAR
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameikaribisha Kampuni ya Al Nakhil kutoka nchini Dubai kuitumia fursa ya kuja kuekeza hapa Zanzibar katika sekta ya utalii.
Dk. Shein alitoa maelezo hayo wakati alipofanya mazungumzo na Sheikh Ali Rashid Lootah Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Nakhil kutoka nchini Dubai Ikulu mjini Zanzibar. Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo wa Kampuni kubwa ya ujenzi ya Al Nakhil ya nchini Dubai kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kutoa ushirikiano wake mkubwa na kuweka mazingira mazuri katika kuhakikisha azma ya Kampuni hiyo inafikiwa.
Dk. Shein alimueleza Mwenyekiti huyo kuwa Zanzibar ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya Utalii na iko tayari kutoa ushirikiano wake kwa Kampuni hiyo hasa ikizingatiwa kuwa ina uzoefu na uwezo mkubwa katika harakati hizo. Aidha, Rais Dk. Shein alimueleza Mwenyekiti huyo juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya utalii sambamba na hatua zilizofikiwa katika kuhakikisha idadi ya watalii imeongezeka.
Hivyo, Rais Dk. Shein aliendelea kusisitiza haja ya kuanzishwa kwa usafiri wa anga hasa kwa kutumia Kampuni ya ndege ya Emirates ambapo kati ya Zanzibar na Dubai, ambapo hatua hiyo itaimarisha na kuongeza idadi ya watalii na kuwasaidia wafanyabiashara na wasafiri wengine.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Nakhil ya Dubai, Sheikh. Ali Rashid Lootah, akiwa na Ujumbe wake,Mohammed Rashed na Masoud Mbarouk, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar, leo 3/12/2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Nakhil ya Nchini Dubai, Sheikh.Ali Rashid Lootah, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 3/12/2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Al Nakhil ya Nchini Dubai, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo.Sheikh. Ali Rashid Lootah,kulia kwa Sheikh.Ali ni Ndg.Mohammed Rashed.(Picha na Ikulu)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA AL NAKHIL YA DUBAI IKULU ZANZIBAR
yaani makala yote RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA AL NAKHIL YA DUBAI IKULU ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA AL NAKHIL YA DUBAI IKULU ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/rais-dkt-shein-azungumza-na-mwenyekiti.html
0 Response to "RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA AL NAKHIL YA DUBAI IKULU ZANZIBAR"
Post a Comment