Nafasi za kazi ya Ualimu

Nafasi za kazi ya Ualimu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Nafasi za kazi ya Ualimu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Nafasi za kazi ya Ualimu
kiungo : Nafasi za kazi ya Ualimu

soma pia


Nafasi za kazi ya Ualimu

NAFASI ZA KAZI KWA SKULI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR


Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Skuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

1. Walimu wa Skuli za Maandalizi:

WILAYA ZA UNGUJA
WILAYA NAFASI
KASKAZINI ‘A’ 15
KASKAZINI ‘B’ 6
MAGHARIBI ‘A’ 4
MAGHARIBI ‘B’ 5
KATI 9
KUSINI 5
WILAYA ZA PEMBA
MKOANI 7
CHAKE CHAKE 4
WETE 4
MICHEWENI 11

Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu fani ya Ualimu wa Maandalizi katika ngazi ya Cheti kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

2. Walimu wa Skuli za Msingi:

WILAYA ZA UNGUJA
WILAYA NAFASI
KASKAZINI ‘A’ 2
KASKAZINI ‘B’ 2
MAGHARIBI ‘A’ 3
MAGHARIBI ‘B’ 3
KATI 3
KUSINI 2
WILAYA ZA PEMBA
MKOANI 5
CHAKE CHAKE 1
WETE 2
MICHEWENI 4


Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Diploma ya Msingi (Diploma in Primary Education) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

3. Walimu wa Skuli za Sekondari:

WILAYA ZA UNGUJA
WILAYA NAFASI
KASKAZINI ‘B’ 2
KUSINI 2
WILAYA ZA PEMBA
MKOANI 3
CHAKE CHAKE 2
WETE 2
MICHEWENI 3

Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amesomea Shahada ya Ualimu katika masomo ya Histroy, English na Kiswahili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4. Mwalimu wa Sayansi Chake Chake Pemba “Nafasi 4”
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amesomea Diploma ya Ualimu wa Sayansi au awe amefaulu vizuri elimu ya Kidato cha Sita katika masomo ya Chemistry, Biology au Physics

5. Muhudumu Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata cheti cha uhudumu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Habari na Mawasiliano (ICT) Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Habari na Mawasiliano’ (ICT) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo ya Ualimu. 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Muombaji anaombwa kuiainisha Wilaya anayoiomba 
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 26 Mei, 2017 wakati wa saa za kazi.


Hivyo makala Nafasi za kazi ya Ualimu

yaani makala yote Nafasi za kazi ya Ualimu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Nafasi za kazi ya Ualimu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/nafasi-za-kazi-ya-ualimu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Nafasi za kazi ya Ualimu"

Post a Comment