NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI

NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI
kiungo : NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI

soma pia


NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI



NA LUSUNGU HELELA-MWANZA.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani  ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya  Kome  na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila kulazimishwa.
Kauli hiyo ameitoa  wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya  Msitu wa Shigala ulioko Kome Mchangani ambayo ni kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dkt. Charles Tizeba amemueleza  Naibu Waziri hiyo kuwa kumekuwepo na changamoto ya ulipaji  tozo kubwa hata kama mtu ana eneo dogo na ndipo wananchi walilazimika kugoma kulipa tozo hiyo kwa lengo la kupata msaada zaidi.

Amefafanua kuwa mtu anayemiliki hekari moja  anatakiwa kulipa Tsh.425,000 kwa mwaka lakini hata mtu anayemikili eneo dogo la mita 20 naye anatakiwa kulipa kama wa hekari moja  kitendo kilichowafanya wananchi hao kushindwa kulipa na kusubili maelekezo ya wizara husika.
Mmoja wa wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi hiyo,Juma Ramadhani amemwomba Naibu Waziri kuangalia upya sheria hiyo ili wananchi wapate nafuu ya kulipa na serikali iweze kupata mapato yake.

Kaimu Meneja wa TFS Kanda ya Ziwa, Thomas Moshi amesema kuwa tozo hizo zipo kwa mujibu wa sheria kinachotakiwa ni wananchi kulipa na siyo kugomea kulipa tozo hizo na wanapofanya hivyo wanakwenda kinyume na matakwa ya sheria ya hifadhi ya misitu.

Kanyasu amewahakikishia wananchi hao kuwa suala hilo atalipatia majibu kwa haraka lakini amewataka watu wanaomiliki hekari moja  kulipa tozo hizo kwa wakati na wale wenye maeneo madogo madogo wajiunge katika vikundi ili waweze kuilipa pesa hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akizungumza na  wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kuwa watalipa tozo za serikali bila kulazimishwa alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
2
 Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akizungumza na wananchi wa Jimboni kwake  kwenye mkutano wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wa kutatua kero za  wananchi wanaoishi ndani ya  Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  katika kijiji cha Kisaba na Bugombe
3
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Buhama kata ya Buhama, Thomas Sabuni, akizungumza  na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kabala ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ikiwa lengo  kutatua kero za wananchi wa Kisiwa hicho wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya katika eneo la Kome mchangani.
4
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akiteta jambo na Meneja wa Shamba la Buhindi , Ayoub Kigongwira wakati wa  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.



Hivyo makala NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI

yaani makala yote NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/naibu-waziri-kanyasu-awataka-wananchi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI"

Post a Comment