title : NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA UWT ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE
kiungo : NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA UWT ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE
NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA UWT ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu mpya wa Zanzibar wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT), Tunu Juma Kondo, amesema atahitumikia jumuiya hiyo kwa hekima na busara ili kutimiza kwa vitendo malengo ya CCM na Jumuiya hiyo. Amesema baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo ametambua kuwa siasa ni hekima na busara hivyo katika utendaji wake atafanya kwa misingi hiyo kwa uadilifu mkubwa.
Hayo aliyasema jana wakati akizungumza na wanajumuiya wa UWT katika ukumbi wa CCM kisiwandui,Naibu huyo alisema hakutarajia kushika nafasi hiyo na kwamba utaratibu wa chama ni mzuri wa kuwateua viongozi bila ya ubaguzi Katika maelezo yake Naibu huyo alisema CCM haina ubaguzi na kwamba inazingatia utendaji wa mtu na si vinginevyo akitoa mfano alisema kwa upande wake hakutarajia kuwa siku moja atapewa jukumu kama hilo.
"Nashukuru UWT kwa kuridhia jina langu lipelekwe katika uongozi wa juu wa chama hivyo sina budi kuwashukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM,Dk.Bashiru Ally,kamati ya Halmashauri Kuu kwa kuniamini na wameonesha imani kubwa kwangu,"alisema Naibu Katibu Mkuu huyo Tunu aliwataka wanajumuiya hiyo kumpa ushirikiano katika utendaji wake na amewataka wakumbuke kuwa siku za mbele kuna uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kwamba wao ndio wapiganaji hivyo wanapaswa kushirikiana.
NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CCM Zanzibar Khadija Kabir mara baada ya kuwasili Zanzibar kwa mara ya kwanza toka alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.
NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akifurahia na wanachama wa UWT katika mapokezi hayo.
NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akizungumza na wanajumuiya wa UWT katika ukumbi wa CCM Kisiwandui
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA UWT ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE
yaani makala yote NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA UWT ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA UWT ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/naibu-katibu-mkuu-mpya-wa-uwt-zanzibar.html
0 Response to "NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA UWT ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE"
Post a Comment