title : MKURUGENZI ALIYETUMIA FEDHA KINYUME NA MWONGOZO ATUMBULIWA
kiungo : MKURUGENZI ALIYETUMIA FEDHA KINYUME NA MWONGOZO ATUMBULIWA
MKURUGENZI ALIYETUMIA FEDHA KINYUME NA MWONGOZO ATUMBULIWA

Mwambawahabari
RAIS John Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Butiama, Solomon Ngiliule kutokana na kutumia fedha kinyume na miongozo iliyowekwa.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofanya ziara Mkoani Mara, kubaini watendaji wa halmashauri kushindwa kusimamia vyema meneo yao ya kazi katika miradi ya maji na afya.
Akitangaza utenguzi huo leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo amemwelekeza Katibu Mkuu TAMISEMI ,kumchukulia hatua stahiki mweka hazina aliyehusika wakati wa matumizi mabaya yaliyofanyika ya fedha za Serikali.
"Nawataka watendaji wote walio chini ya Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia Kanuni za Utumishi wa Umma na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa maslahi mapana ya wananchi na taifa letu, "amesema.
Amesema asilimia 20 ya fedha za bajeti ya serikali imeelekezwa Tamisemi, hivyo wafanye kazi kwa ufanisi na kuzingatia maadili.
"Niwasihi wakurugenzi wengine wote ambao wamepewa dhamana na Rais, tunawapima kwa utendaji wao wa kazi...na wale ambao watabainika hawawndani na kasi hii ya sasa lakini kipaumbele chetu ni kuhakikisha thamani ya fedha na suala la kujali utu na uwajibikaji katika meneo yao ya kazi ni jambo la msingi, "amesema.
Jafo amefafanua kuwa dhamana waliopewa wakuu wa Idara, wakurugenzi ni kubwa hivyo wahakikishe wanafanya kazi zao kwa weledi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Amesema kila mtu anapaswa kuhakikisha anafanya kazi kwa maslahi ya wananchi na si ya mtu binafsi.
Ameongeza kuwa, hadi sasa serikali inafanya uchunguzi na kwamba watakaobainika kuhusika katika utumiaji huo wa fedha hawatasita kuwachukulia hatua.
Hivyo makala MKURUGENZI ALIYETUMIA FEDHA KINYUME NA MWONGOZO ATUMBULIWA
yaani makala yote MKURUGENZI ALIYETUMIA FEDHA KINYUME NA MWONGOZO ATUMBULIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKURUGENZI ALIYETUMIA FEDHA KINYUME NA MWONGOZO ATUMBULIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/mkurugenzi-aliyetumia-fedha-kinyume-na.html
0 Response to "MKURUGENZI ALIYETUMIA FEDHA KINYUME NA MWONGOZO ATUMBULIWA"
Post a Comment