Mkufunzi kutoka Japan kushuhudia ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship’

Mkufunzi kutoka Japan kushuhudia ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship’ - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mkufunzi kutoka Japan kushuhudia ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship’, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mkufunzi kutoka Japan kushuhudia ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship’
kiungo : Mkufunzi kutoka Japan kushuhudia ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship’

soma pia


Mkufunzi kutoka Japan kushuhudia ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship’


MKUFUNZI wa Riadha kutoka Japan, Ayane Sato, anatarajiwa kushuhudia Mashindano ya Riadha ya Taifa ya Wazi ya Ngorongoro ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship 2018’ yanayotarajiwa kurindima Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha, Ijumaa Desemba 14 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavala, mkufunzi huyo ambaye yuko nchini kwa miaka miwili akijitolea, atashuhudia mashindano hayo ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kikazi, ikiwamo kuwanoa wanariadha mbalimbali hapa nchini.Zavala, alisema itakuwa ni fursa pekee kwa Sato kujionea vipaji mbalimbali vya wanariadha kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani, jambo litakalomrahishia majukumu yake.

Ujio wa Sato ni kutokana na mahusiano mazuri kati ya Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Maendeleo (JICA), na RT.Mashindano ya wazi ya Taifa ambayo yamewezeshwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), yatashirikisha mbio za Mita 100, Relay 100×4, 200, 400, Relay 400×4, 800, 1,500, 5,000 na Mita 10,000, Kuruka Juu, Kuruka Chini, Miruko Mitatu, Kurusha Mkuki, Tufe na Kisahani kwa wanaume na wanawake.

Washindi watakaofanya vizuri watazawadiwa zawadi za fedha na medali, ambako mshindi wa kwanza atapata Medali ya Dhahabu na kitita cha Sh. 150,000 wa pili Medali ya Fedha na Sh. 100,000 huku wa tatu akiondoka na Medali ya Shaba na Sh. 50,000.Pia watapata fursa ya kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwamo Japan, kusaka viwango vya kufuzu mashindano ya kimataifa ikiwamo World Championship na Olimpiki.

Sato katikati siku akitambulishwa kwa waandishi wa habari. Kulia kwake ni Katibu Msaidizi RT, Ombeni Zavala na Mjumbe RT, Tullo Chambo
 



Hivyo makala Mkufunzi kutoka Japan kushuhudia ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship’

yaani makala yote Mkufunzi kutoka Japan kushuhudia ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship’ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mkufunzi kutoka Japan kushuhudia ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship’ mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/mkufunzi-kutoka-japan-kushuhudia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mkufunzi kutoka Japan kushuhudia ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship’"

Post a Comment