title : VETA yaanzisha ushirikiano na Chuo cha Henan-China
kiungo : VETA yaanzisha ushirikiano na Chuo cha Henan-China
VETA yaanzisha ushirikiano na Chuo cha Henan-China
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesaini makubaliano ya kuanzisha ushirikiano kati yake na Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo lengo la kuboresha utoaji wa mafunzo kwa njia ya kutembeleana na kubadilishana ujuzi na maarifa kwa walimu na wanafunzi na shughuli zingine za kitaaluma.
Makubaliano hayo ya awali yaliafikiwa na kusainiwa leo (tarehe 20 Desemba 2018) kati ya Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo, Profesa Dou Ruimu kwa upande mmoja na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dr. Pancras Bujulu kwa upande mwingine na kwamba yatafuatiwa na utiaji saini wa Waraka wa Makubaliano (MoU) siku za mbeleni.
Utiaji saini wa makubaliano ya awali uishuhudiwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Noel Mbonde na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET Board), Peter Maduki, wawakilishi wa Chuo cha Henan na Wajumbe wa Menejimenti ya VETA.
VETA ina nia ya kuimarisha mafunzo katika sekta ya kilimo na miongoni mwa malengo yake ni kukiimarisha na kukiboresha chuo cha VETA Kihonda ili kiweze kubobea na kuwa kituo bora cha mfano katika mafunzo ya ufundi stadi kwenye sekta ya kilimo.
Kabla ya kusaini makubaliano, ujumbe wa watu sita kutoka Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo ukiwahusisha watendaji wakuu na wataalam mbalimbali umekuwepo nchini tangu Jumanne tarehe 18 Desemba 2018 ambapo ulifanya majadiliano na Menejimenti ya VETA Makao Makuu, ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt Pancras Bujulu na Jumatano, tarehe 19 Desemba 2018 ulitembelea ofisi ya VETA Kanda ya Mashariki, kisha chuo cha VETA Kihonda na kujionea karakana, mashine na vifaa mbalimbali vinavyotumika kufundishia fani ya Ufundi wa Zana za Kilimo (Agro-mechanics), mafunzo ambayo yanagusa sekta ya kilimo ambayo ndio mkondo wa chuo cha Henan.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu (wa pili kutoka kulia, waliokaa) na Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo, Profesa Dou Ruimu (wa pili kutoka kushoto,waliokaa) wakisaini makubaliano ya awali ya ushirikiano kati yao. Wa kwanza kulia, waliokaa ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Noel Mbonde na wa kwanza kushoto waliokaa naye ni Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan, Chen Yueying.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu (wa pili kutoka kulia, mstari wa mbele) na Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo, Profesa Dou Ruimu (wa pili kutoka kushoto, mstari wa mbele) wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya awali ya ushirikiano kati yao. Wa kwanza kulia, mstari wa mbele ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Noel Mbonde na wa kwanza kushoto, mstari wa mbele naye ni Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan, Chen Yueying. Wengine ni wajumbe wa Menejimenti ya VETA na Wawakilishi wa chuo cha Henan.
Hivyo makala VETA yaanzisha ushirikiano na Chuo cha Henan-China
yaani makala yote VETA yaanzisha ushirikiano na Chuo cha Henan-China Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VETA yaanzisha ushirikiano na Chuo cha Henan-China mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/veta-yaanzisha-ushirikiano-na-chuo-cha.html
0 Response to "VETA yaanzisha ushirikiano na Chuo cha Henan-China"
Post a Comment