title : Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mtumishi wa afya
kiungo : Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mtumishi wa afya
Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mtumishi wa afya
Mtumishi wa Wizara ya Afya kitengo cha maabara na mkazi wa Mpwapwa mkoani Dodoma Mbwana Saidi Mbela , ameibuka mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 za Tigo Jigiftishe na kukabidhiwa zawadi yake jijini Da es Salaam.
Mbela anakuwa ni mshindi wa tatu wa zawadi ya shilingi milioni 10 ambayo hutolewa kila wiki kwa mshindi mmoja kupitia Promosheni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe. Milioni 10 ya kwanza ilichukuliwa na David Mmuni huku ya pili ikienda kwa Iyaka Seifu Muinga.
Mbela aliungana na washindi wengine wanne ambao ni washindi wa kila siku ambao walikabidhiwa shilingi milioni moja moja .Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake katika hafla iliyofanyika eneo la Chamazi jijini Dar es Salaam, Mbela alisema alipigiwa simu kuwa ameshinda akiwa likizo jijini Dar es Salaam ambapo alikuja kumtembela shangazi yake.
“Niliamua kutumia likizo yangu kuja jijini Dar es Salaam kumsalimia shangazi yangu. Nilipofika tu nyumbani kwake Chamazi, nikapigiwa simu ya kuambiwa kuwa nimekuwa mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10,” anasema. Mbela aliishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo na kusema kuwa atatumia fedha hizo kumalizia nyumba yake.

Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Mbwana Saidi Mbela (wa kwanza kulia) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Shadya Bakari (kulia) wa Tigo katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam. Katikati ni Verykeys Julius kutoka Kitengo cha Biashara Tigo
Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Mbwana Saidi Mbela (wa tatu kulia) akipongezwa na washindi wa kila siku wa shilingi milioni moja moja pamoja na wafanyakazi wa Tigo muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake katika halfa iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam
Mmoja wa washindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Theresia Philipo (wa kwanza kulia) akilia kwa furaha wakati akikadihiwa mfano wa yenye thamani ya shilingi milioni moja na Shadya Bakari (wa kwanza kushoto) kutoka Tigo katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam. Katikati ni Verykeys Julius kutoka Kitengo cha Biashara Tigo
Hivyo makala Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mtumishi wa afya
yaani makala yote Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mtumishi wa afya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mtumishi wa afya mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/milioni-10-za-tigo-jigiftishe-zaenda.html
0 Response to "Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mtumishi wa afya"
Post a Comment