title : KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUFANYIKA TAREHE 10 NA 11 JANUARI, 2019 ZANZIBAR
kiungo : KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUFANYIKA TAREHE 10 NA 11 JANUARI, 2019 ZANZIBAR
KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUFANYIKA TAREHE 10 NA 11 JANUARI, 2019 ZANZIBAR

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inapenda kuwataarifu wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa, tarehe 10 na 11 Januari, 2019 kutakuwa na kikao cha kawaida cha Baraza la Vyama vya siasa, kitakachofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Bima Zanzibar uliopo eneo la Madema barabara ya Michenzani mjini Unguja, Zanzibar.
Awali kikao hicho ambacho kilitarajiwa kufanyika tarehe 21 na 22 Desemba, 2018 kiliahirishwaili kuwezesha Vyama vya Siasa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mdogo wa tarehe 19 Januari, 2019.
Aidha kikao cha Kamati ya Uongozi kitafanyika tarehe 8 Januari, 2019 kufanya maandalizi ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa. Kwa kuwa wagombea karibu wote wamepita bila kupingwa, Mkuu wa Sekretarieti ya Baraza la Vyama vya Siasa ambaye ni Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis Mutungi na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Bw. John Shibuda wameshauriana na kukubaliana kuwa, ni vyema kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kifanyike mapema, ili kuwezesha Baraza kuandaa maoni yake kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na kuyawasilisha katika Kamati husika ya Bunge inayooanza shughuli zake tarehe 14 Januari, 2019.
Kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kitatanguliwa na Semina kwa wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kuhusu utaratibu wa kutunga Sheria, itakayotolewa na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Semina itafanyika tarehe 09 Januari, 2019 katika Ukumbi wa ofisi ndogo za Bunge Zanzibar zilizopo eneo la Tunguu.
Baadhi ya ajenda za kikao zitakazojadiliwa ni pamoja na taarifa mbalimbali zinazohusu Baraza la Vyama vya Siasa, kujadili muswaada wa Sheria mpya ya Vyama vya Siasa na uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Baraza.
Monica L. Mnanka
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Elimu kwa Umma
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Hivyo makala KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUFANYIKA TAREHE 10 NA 11 JANUARI, 2019 ZANZIBAR
yaani makala yote KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUFANYIKA TAREHE 10 NA 11 JANUARI, 2019 ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUFANYIKA TAREHE 10 NA 11 JANUARI, 2019 ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/kikao-cha-baraza-la-vyama-vya-siasa_28.html
0 Response to "KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUFANYIKA TAREHE 10 NA 11 JANUARI, 2019 ZANZIBAR"
Post a Comment