title : TCAA yajibu mapigo ya Fastjet. yakanusha kuibania kuingiza ndege
kiungo : TCAA yajibu mapigo ya Fastjet. yakanusha kuibania kuingiza ndege
TCAA yajibu mapigo ya Fastjet. yakanusha kuibania kuingiza ndege
Hussein Ndubikile
Mwamba wa habari
Mamalaka ya Usafiri a Anga nchini (TCAA) imekanusha taarifa za upotoshaji zinazoeleza kuwa mamlaka hiyo inalibana Shirika la Ndage la Fasjet kuingiza ndege mpya Disemba 22 mwaka huu badala yake imebainisha kuwa ilipokea maombi ya kuleta ndege hiyo Disemba 24 huku ikisisitiza maombi hayo yanafanyiwa kazi.
Mamlaka hiyo imebainisha kuwa ilikuwa halina taarifa ya kupokea ndege badala yake iliwafikia usiku wa tarehe hiyo na kusisitiza inaendelea kuyafanyia kazi maombi yaliyowasilishwa.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Shitika la Utangazi la Uingereza (BBC) kutoa taarifa zinazoeleza mamlaka hiyo kuiwekea ugumu kampuni hiyo kuingiza ndege mpya nchini kutoa huduma ya usafiri.
Aidha, TCAA imesema Fasjet inadaiwa zaidi ya Sh bilioni sita na mamlaka zinazotoa huduma ya usafiri wa anga pamoja na wasambazaji.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Hamza Johari wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na taarifa za upotoshaji zilizotolewa na shirika hilo.
Amesema kuwa awali shirika hilo lilikuwa likimilikiwa na Mwingereza na baada kuliacha wazawa walinunua hisa akiwemo Mwqenyekiti mtendaji wa wa shirika hilo akiwemo Lawrence na kuanza kuliendesha na kubainisha kuwa baada ya kutokea matatizo Meneja usimamizi wa ndege hizo alijiuzulu na ndiye aliyekuwa akijua masuala ya ndege hivyo mamlaka hiyo haiwezi kuiruhusu ndege hiyo kuruka bila mtu huyo kuwepo.
Amesisitiza kuwa shirika hilo lina matatizo makubwa yanayolifanya lishindwe kuendelea kutoa huduma ya usafiri wa anga na kwamba walitoa 28 ya kulisimamisah lisiendele kutoa huduma walishajiridhisha kampuni hiyo kuwa na madeni pamoja na ndege isiyoweza kutoa huduma ya uhakika.
Amefafanua kuwa moja ya masharti waliyolipatia shirika hilo ni kumteua mtu mwenye utalaamu wa masuala ya anga ambapo mwenyekiti wa shirika hilo alimteua Lawrence Marsha kuwa meneja usimamizi.
Hamza amesema sharti jingine walilotoa kwa Fasjet ni kuwasilisha andiko la kibiashara likiwa na mchanganuo wa upatikanaji wa fedha za uendeshaji.
Katika hatua nyingine, amekanusha taarifa zilizotolewa na mtandao wa Jamii Forum kuwa TCC inalipendelea Shiirika la Ndege Nchini (ATCL) na kwamba maneno hayo hayana ukweli bali kinachotakiwa ni kila shirika kufuata sheria wa anga kwa ajili ya usalama wa abiria wanaotumia usafiri wa anga.
" TCAA tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria za anga hatupendelei shirika lolote ndio maana kuna kipindi hata ndege za ATCL zilizuiwa kufanya safari za anga kutokana kutokidhi sheria na taratibu zinazoongoza usafiri wa anga," amesema Johari.
Hivyo makala TCAA yajibu mapigo ya Fastjet. yakanusha kuibania kuingiza ndege
yaani makala yote TCAA yajibu mapigo ya Fastjet. yakanusha kuibania kuingiza ndege Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TCAA yajibu mapigo ya Fastjet. yakanusha kuibania kuingiza ndege mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/tcaa-yajibu-mapigo-ya-fastjet-yakanusha.html
0 Response to "TCAA yajibu mapigo ya Fastjet. yakanusha kuibania kuingiza ndege"
Post a Comment