title : Equinor kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi wao waliowafadhili.
kiungo : Equinor kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi wao waliowafadhili.
Equinor kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi wao waliowafadhili.
Equinor Tanzania inaona fahari kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi kumi na tatu miongoni mwa wanafunzi wake wengi inaowafadhili ambao wamekuwa wakichukua masomo ya shahada- ya pili (Uzamili) katika Geoscience and Engineering.
Wanafunzi wanaohitimu wamekuwa wakifadhiliwa chini ya programu ya ufadhili wa Equinor Tanzania unaojulikana kama Angola Tanzania Higher Education (ANTHEI). Programu hii ya ufadhili ya ANTHEI kutoka kwa Equinor ni programu ambayo inatoa ufadhili kamili kwa hadi kufikia wanafunzi kumi kila mwaka kusomea shahada ya pili katika masomo ya (Utafiti wa Petroli) Petroleum Geoscience na Uhandisi wa Petroli (Petroleum Engineering) katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Norway (Norwegian University of Science and Technology) (NTNU) kinachofanya kazi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Da es salaam (UDSM).
Wanafunzi wanaohitimu wamekuwa wakifadhiliwa chini ya programu ya ufadhili wa Equinor Tanzania unaojulikana kama Angola Tanzania Higher Education (ANTHEI). Programu hii ya ufadhili ya ANTHEI kutoka kwa Equinor ni programu ambayo inatoa ufadhili kamili kwa hadi kufikia wanafunzi kumi kila mwaka kusomea shahada ya pili katika masomo ya (Utafiti wa Petroli) Petroleum Geoscience na Uhandisi wa Petroli (Petroleum Engineering) katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Norway (Norwegian University of Science and Technology) (NTNU) kinachofanya kazi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Da es salaam (UDSM).
Programu hii imeandaliwa kwa namna kwamba mwanafunzi atatumia mwaka mmoja nchini Norway na kukamilisha mwaka wa mwisho wa masomo ya shahada ya pili katika chuo cha UDSM. Kwa mujibu wa hati ya makubaliano iliyosainiwa na Equinor, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na NTNU mpango huu wa udhamini chini ya Equinor ulianza mwaka 2012 na utaendelea mpaka 2019.
Jumla ya wahandisi wa Petroli wapatao 42 (Wahandisi wa Uzalishaji, Uhifadhi na wahandisi wa Uchimbaji) wahandisi 16 wa Utafiti wa Petrioli (Geology, Petrophysicis na Geophysics) na wahandisi 6 wa usimamizi wa miradi wameshasajiliwa mpaka sasa.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen akizungumza jana na waandishi wa habari na wanafunzi waliohitimu shahada ya pili (Uzamili) masomo ya Petroleum Geoscience and Engineering waliodhaminiwa masomo na Kampuni ya Equinor Tanzania kupitia mpango wa ANTHEI. Jumla ya wanafunzi kumi na tatu walihitimu ambao wataweza kufanya utafiti na kufundisha uwezo ndani ya sekta ya Mafuta na Gesi, na utunzaji wa hesabu na fedha katika sekta hiyo.
Mhitimu, Bertha Ngereja akitoa shukurani zake kwa niaba ya wenzake kwa wafadhili Equinor Tanzania, ANTHEI, UDSM na NTNU kwa kuwawezesha kupata shahada ya pili ya masomo mbalimbali yanayohusu Mafuta na Gesi. Sherehe za mahafali zilifanyika jana kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.
Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dr. Mette H. Ottoy akizungumza jana na waandishi wa habari na wanafunzi waliohitimu shahada ya pili (Uzamili) masomo ya Petroleum Geoscience and Engineering waliodhaminiwa masomo na Kampuni ya Equinor Tanzania kupitia mpango wa ANTHEI. Jumla ya wanafunzi kumi na tatu walihitimu ambao wataweza kufanya utafiti na kufundisha uwezo ndani ya sekta ya Mafuta na Gesi, na utunzaji wa hesabu na fedha katika sekta hiyo.
Mhitimu, Masolwa Kasongi akipokea cheti cha kuhitimu shahada ya pili ya Geoscience and Engineering jana kwenye sherehe ya mahafali zilizofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.
Hivyo makala Equinor kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi wao waliowafadhili.
yaani makala yote Equinor kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi wao waliowafadhili. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Equinor kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi wao waliowafadhili. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/equinor-kusimamia-sherehe-za-mahafali.html
0 Response to "Equinor kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi wao waliowafadhili."
Post a Comment