title : TAASISI YA USTAWI WA JAMII WANYAKUA TUZO ZA NBAA KWA MARA YA TATU
kiungo : TAASISI YA USTAWI WA JAMII WANYAKUA TUZO ZA NBAA KWA MARA YA TATU
TAASISI YA USTAWI WA JAMII WANYAKUA TUZO ZA NBAA KWA MARA YA TATU
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
BODI ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) watoa Tuzo kwa Taasisi, Makampuni pamoja na mashirika yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2018 iliyofanyika Bunju jijini Dar es salaam.
Akipokea Tuzo hiyo Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii Athuman Senzota amesema ni kwa Mara ya tatu wananyakua Tuzo hiyo ambapo vilikua vyuo viwili kwenye kinyang'anyiro cha Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu na Taasisi ya ustawi kuwa washindi wa pili huku nafasi ya kwanza kushika chuo cha Mzumbe.
Senzota ameeleza kuwa Tuzo hiyo waliyoipata inaonyesha jinsi gani Taasisi ya Ustawi wa Jamii ni waadilifu na wachapakazi wa hali ya juu katika kutunza na kutumia pesa za Umma Kikamilifu kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha 2018.
Hata hivyo amefafanua kuwa waliweza kufikia viwango ambavo viliwawezesha kushinda Tuzo ambapo ili uweze kushinda Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi ilizingatia viwango vya uwasilishaji kufikia 75% ya Mapato kwa mwaka wa fedha 2018 .
Na Tuzo hiyo imekua chachu kwa Taasisi ya ustawi wa jamii inayofanya tuendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa Mapato ili kusaidia jamii na maslahi kwa nchi kwa ujumla.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Zena Mabeyo akipokea Tuzo ya uwasilishaji wa Mapato ya fedha katika nafasi ya Taasisi ya elimu ya juu na Vyuo vikuu zilizoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) kwa mwaka 2018 jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii CPA Athuman Senzota akizungumza na waandishi wa habari baada ya kushinda Tuzo ya uwasilishaji wa Mapato ya fedha kwa mwaka 2018.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TAASISI YA USTAWI WA JAMII WANYAKUA TUZO ZA NBAA KWA MARA YA TATU
yaani makala yote TAASISI YA USTAWI WA JAMII WANYAKUA TUZO ZA NBAA KWA MARA YA TATU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI YA USTAWI WA JAMII WANYAKUA TUZO ZA NBAA KWA MARA YA TATU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/taasisi-ya-ustawi-wa-jamii-wanyakua.html
0 Response to "TAASISI YA USTAWI WA JAMII WANYAKUA TUZO ZA NBAA KWA MARA YA TATU"
Post a Comment