KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA

KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA
kiungo : KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA

soma pia


KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA

WAZIRI wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amesema ni vyema Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuanza kuwekeza katika kubuni teknolojia za kisasa na kuzalisha mashine za kurahisisha shughuli za viwanda nchini.

Kakunda aliyasema hayo alipotembelea banda VETA katika Maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere-Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema kutokana na mkakati wa serikali kwenda katika uchumi wa kati kupitia viwanda, VETA  inawajibu wa kuzalisha nguvu kazi yenye uwezo wa kubuni teknolojia ambazo zitarahisisha kufanya uchakataji wa malighafi zinazolishwa nchini.

 Kakunda amesema kuwa mali ghafi zikichakatwa nchini zitasaidia kuongeza mnyororo wa thamani wa malighafi hizo na hatimaye kuwasiadia wakulima kunufaika na kilimo wanachokifanya.

“VETA mna nafasi kubwa nchini katika maendeleo ya viwanda na serikali inawategemea katika uzalishaji wa teknolojia na nguvu kazi ili kusaidia kusukuma maendeleo hayo,” alisema.

Maonesho ya tatu ya bidhaa za viwanda yanafanyika katika viwanja vya Sabasaba kuanzia tarehe 5 hadi 9 Desemba 2018.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda akiangalia Kibuda cha kuchakata mihogo wakati alipotembelea banda la VETA katika maonesho ya Tatu ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji  Joseph Kakunda akipata maelezo kutoka kwa Afisa habari wa VETA David Edward wakati alipotembelea banda la VETA katika maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda akiangalia bidhaa zinazozalishwa na VETA wakati alipotembelea maonesho ya Tatu ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.


Hivyo makala KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA

yaani makala yote KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/kakunda-aitaka-veta-kuwekeza-kwenye.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA"

Post a Comment