Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma

Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma
kiungo : Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma

soma pia


Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma



Na Nuru Mwasampeta

Kufuatia ziara ya Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoifanya hivi karibuni katika eneo la Ihumwa ambako ujenzi wa Mji wa Serikali unaendelea na kubaini uhaba wa kokoto katika ujenzi huo, leo Disemba 30, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akifuatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Anthony Mavunde wamefanya ziara ya kushtukiza kwenye maeneo yanayochimba kokoto hizo na kubaini madudu.

Naibu Mawaziri hao wamebaini machimbo ya kokoto yakiwa yamefungwa kwa madai kuwa wafanyakazi wako likizo, zikiwemo mashine za kusagia mawe hayo zikiwa zimeharibika kwa takribani miezi mitatu na hivyo kupelekea uzalishaji kusimama.

Akizungumza katika eneo hilo la machimbo, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema anashangazwa kuona kuwa watumishi katika mgodi wa kokoto wanakwenda likizo wakati mahitaji ya kokoto ni makubwa na soko la uhakika. “Mmechukua zabuni kwa ajili ya kusambaza kokoto kutoka kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),na kampuni ya MZINGA wenye uhitaji mkubwa kwa ajili ya ujenzi wa mji wa Serikali unaoendelea halafu mnadai mko likizo,?” amehoji Biteko.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Laroy Aggregate Co. Ltd , Biteko amemtaka mkurugenzi huyo aliyefahamika kwa jina la Joel Mchovu kuhakikisha kuwa, ifikapo Januari 2, 2019 kokoto ziwe zimezalishwa na kusambazwa kwa wahitaji kama walivyokubaliana ili ujenzi uendelee kwa kasi iliyokusudiwa.

Aidha, amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa juhudi na weledi mkubwa ili kuzalisha kiasi kinachotosheleza mahitaji vinginevyo oda zitahamishwa na kupewa kampuni za zinazozalisha kokoto zilizopo Chalinze ambazo zinaonesha uwezo mkubwa katika uzalishaji wa kokoto.

Fundi wa mashine katika mgodi wa WADI Gao Peng (wa pili kushoto), akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Wa pili kutoka kulia) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde (wa Kwanza kushoto) walipofanya ziara katika machimbo hayo ili kujionea kinachoendelea, wa kwanza kulia ni Afisa Madini wa Mkoa wa Dodoma mhandisi Jonas Mwano. 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika machimbo ya kokoto ya kampuni ya Laroy Aggregate Co. Ltd, Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde na kushoto ni msaidizi wake Kungulu K. Masakala 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko, akitoa tamko la Serikali kwa wachimbaji wa kokoto alipofanya ziara kujionea kinachoendelea katika machimbo hayo baada ya kubainika uhaba wa kokoto katika eneo la ujenzi wa ofisi za Serikali Ihumwa jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) pamoja na Naibu Waziri Ofisi  ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde (Kulia) wakiangalia moja ya kifaa kinachotumika katika kuchoronga mawe kwa ajili ya kokoto ambacho kwa sasa hakifanyi kazi kutokana na kuharibika. Katikati ni Fundi wa mashine katika mgodi wa WADI Gao Peng .



Hivyo makala Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma

yaani makala yote Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/doto-biteko-atoa-maagizo-mazito-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma"

Post a Comment