title : TWASHEREHEKEA MAISHA YA MAMA ma YOHANAMARIA KOKULAMUUKA MUTEMBEI
kiungo : TWASHEREHEKEA MAISHA YA MAMA ma YOHANAMARIA KOKULAMUUKA MUTEMBEI
TWASHEREHEKEA MAISHA YA MAMA ma YOHANAMARIA KOKULAMUUKA MUTEMBEI

mawili akaongea, usingizini kurejea;
tukaita hakuitika; kumbe amehitimisha,
kwa kauli na vitendo, aliposema: “naba ndioo”,
kama anayetwambia kazi ameimaliza,
kwamba saa ilishatimia, atavuka kwenda ng’ambo tupokee kishujaa.
Mama amefaulu, hatulii, twashangilia.
Amebaki shujaa wetu kama Baba alivyokuwa.
Kushughulika na kuelekeza, mahitaji ya wanae kama Mwalimu stadi awezavyo darasa.
Kila mwanae alijisikia amefika na kujiona muhimu kwake,
naye akawa rubani, kutuongoza safarini;
Akatujengea umoja, utuongozao mpaka kesho.
Ukidhihirika kwa jamaa pana, ya waume wa binti zake na wake wa wanae,
watoto na wajukuu, vitukuu na vilembwe.
Ukali twaukumbuka, alishikilia nidhamu,
hakutaka tupotee, kiimani, mila na desturi.
Alisimamia elimu na kuhimiza bidii, hakuwa na mzaha akisema waziwazi:
afadhali msumbuke sasa faida mtaiona baadaye.
Aliiishi nidhamu, akawa mfano kwetu na wajao nyuma yetu.
Ya kwamba maisha bora ni bidii, kutokukata tamaa na kumtegemea Mungu.
Tunaposheherekea mwaka mmoja, twakumbuka ukarimu wake,
Waliomtembelea hawakuondoka, bila chai, chakula na heri kuwaombea
Alithamini mila na desturi
Akajiunga na kina mama, vyamani kijijini na mjini;
Marafiki rika mbalimbali akawagusa watu wengi;
Alikuwa na elimu
kuhimili changamoto,kujadili na wenye elimu mbalimbali bila kubaki nyuma
kipaji chake cha kumbukumbu kilikuwa kitabu cha historia, kilichoandikwa kwa umakini
kukumbuka yaliyojiri, kwa habari za kijamii za furaha na huzuni,
kwa habari za koo, za mila na desturi
Tunamshukuru Mungu tukisherehekea maisha yake. Alivipigana vita vizuri mwendo akaumaliza na imani akailinda.
Shukurani ya pekee itatolewa katika Kanisa la KKKT/NWD Usharika wa Kabale Bukoba, tarehe 18/11/2018
Hivyo makala TWASHEREHEKEA MAISHA YA MAMA ma YOHANAMARIA KOKULAMUUKA MUTEMBEI
yaani makala yote TWASHEREHEKEA MAISHA YA MAMA ma YOHANAMARIA KOKULAMUUKA MUTEMBEI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TWASHEREHEKEA MAISHA YA MAMA ma YOHANAMARIA KOKULAMUUKA MUTEMBEI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/twasherehekea-maisha-ya-mama-ma.html
0 Response to "TWASHEREHEKEA MAISHA YA MAMA ma YOHANAMARIA KOKULAMUUKA MUTEMBEI"
Post a Comment