MWANAMKE AMEUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA

MWANAMKE AMEUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWANAMKE AMEUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWANAMKE AMEUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA
kiungo : MWANAMKE AMEUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA

soma pia


MWANAMKE AMEUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA


Mwanamke mmoja Mkazi wa Kijiji cha China Kata ya Kate wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa, Telestina Silanda (45) ameuawa kwa kuchinjwa na mwili kucharangwa na watu wasiojulikana akiwa amelala nyumbani kwake usiku wa kuamkia jana.

Ndugu wa marehemu, Charles Silanda alidai tukio hilo lilitokea saa mbili usiku watu wasiojulikana waliovalia “kininja” walipovamia nyumba yake (shangazi) na kumshambulia kwa panga na kumchinja.

Alisema hadi wao wanajulishwa tukio hilo na kukimbilia eneo la tukio walikuta shangazi ameuawa na wauaji hao wametoweka katika eneo la tukio. Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Konrad Kauzeni alisema mwanamke huyo aliuawa kinyama, kwa kukatwa miguu yake yote miwili na kuitenganisha na mwili, kichwa na shingo.

Alisema mume wa mwanamke huyo alikuwa amekwenda porini kurina asali kwenye mizinga yake na aliporejea nyumbani alikuta mkewe kauawa kikatili na waliofanya tukio hilo hawajafahamika.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo akisema ataenda kijiji hicho wananchi wapige kura za maoni ili kuwabaini wauaji hao.

Alisema ni jambo lisilokubalika watu kufanya uhalifu mkubwa kiasi hicho na wakaachwa, hivyo kura za maoni zitasaidia kuwanasa wauaji hao ili sheria ichukue mkondo wake. Aliwataka wakazi wa eneo hilo kwenda ofisini kwake kutoa taarifa za siri kwa wale wanaowafahamu


Hivyo makala MWANAMKE AMEUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA

yaani makala yote MWANAMKE AMEUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWANAMKE AMEUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/mwanamke-ameuawa-kwa-kucharangwa-mapanga.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MWANAMKE AMEUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA"

Post a Comment