RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI

RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI
kiungo : RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI

soma pia


RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani 
KAMANDA wa jeshi la polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa anadaiwa kutishiwa na watu wasiofahamika kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS) kuwa watamhamisha kwenye mkoa huo kutokana na kuzuia kuingiza bidhaa za magendo kwenye bandari bubu. Licha ya kitisho hicho amesema,hawezi kulegeza uzi kwani shughuli hizo zinasababisha nchi kukosa mapato kwa kukwepa ushuru.

Akizungumza kwenye kituo cha polisi wilaya ya Bagamoyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kufanikiwa kukamata bidhaa mbalimbali ikiwemo madumu ya mafuta ya kula 4,311 ya lita 20 kila moja na mafuta ya dizeli madumu 52 kwenye oparesheni zinazoendelea mkoani humo.
 "Kwa siku za hivi karibuni mimi pamoja na watendaji wenzangu akiwemo ofisa upelelezi wa mkoa tumekuwa tukitumiwa jumbe za vitisho kupitia simu" “Nitafanya kazi kwa maelekezo ya mkuu wa mkoa, IGP na Rais hivyo siko tayari kufanya kazi kwa maelekezo ya watu wengine ambayo ni kwa maslahi ya mtu binafsi bali kwa maslahi ya nchi"

“Sitishwi na mtu wala sms eti watatuhamisha ama watatupeleka Mlingotini waambieni meseji zao tunazo ,tunazifanyia kazi na tumechukua namba za hawa tuliowakamata kutokana na operesheni hizi kama ni miongoni mwao tutawachukulia hatua kali "alieleza Nyigesa.
 Nae mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisema lazima vyombo vinavyohusika vifuatilie jambo hili ikiwa ni pamoja na mamlaka ya chakula na dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato (TRA).

" Kila mamlaka hapo inapaswa kuhakiki bidhaa hizo ili kujiridhisha kuwa  bidhaa hizi zimeingizwa nchini kwa kufuata taratibu ??na ile ya chakula na dawa kuangalia kama mafuta hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu"alisema Ndikilo.
Katika msako huo pia vifaa vya ujenzi marumaru katoni 200, friji 16, pikipiki moja isiyokuwa na namba bangi kete 512 na pombe ya moshi lita 16 vilikamatwa na watuhumiwa 17 wanaotuhumiwa kuhusika na matukio hayo wanashikiliwa.


Hivyo makala RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI

yaani makala yote RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/rpc-pwani-apewa-vitisho-na-watu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI"

Post a Comment