MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR

MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR
kiungo : MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR

soma pia


MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR



Na Mwashungi Tahir ,Maelezo

Mkurugenzi wa Uwezeshaji Mamlaka ya Udhibi wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar Omar Zubeir Ismail alisema SeriKali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na utafiti wa mafuta na Gesi Asilia kwa njia ya mtetemo kwa kitalu cha Pemba Zanzibar.

Hayo ameyasema leo huko Bandarini Malindi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana kuwasili meli kubwa ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwenye kina kifupi cha maji. 

Aidha alichukua nafasi kwa kuwajuilisha wananchi kazi ya utafiti wa mafuta na gesi Asilia kwa njia ya mtetemo bado inaendelea kwa upande wa kina kifupi cha maji (TRANSITION ZONE 2D SEISMIC SURVEY) katika maeneo ya visiwa hivyo.

“Nachukua nafasi hii kuwajuilisha wananchi kwamba suala la uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ni la muda mrefu na linaweza kufika hadi miaka kumi kukamilika nawaomba muendelee na kazi zenu za kawaida”. Alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema tumuombe Mungu tufanikiwe suala hili kwani likifanikiwa ni la wote kwa maendeleo ya nchi yetu na vizazi vyetu vya hapo baadae. Pia alisema meli zitakazotumika katika zoezi la mtetemo kwa kina kifupi cha maji tayari zimeshawasili nchini kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.

Meli kubwa itakayotumika kurekodi taarifa za mtetemo kwa kina kifupi cha maji wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika maeneo ya Unguja na Pemba ya Stanford Bateleur ikiwa imefunga gati Bandari Malindi ikiwa tayari kuanza kazi hiyo wiki ijayo. 
Nahodha wa meli ya Stanford Bateleur Raul Mendoza akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu meli hiyo inavyofanyakazi ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika kina kifupi cha maji 
Mkurugenzi Uwezeshaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa utafutaji na Uchimabaji wa Mafuta na Gesi AsiliaOmar Zubeir Ismail akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ujio wa meli ya Stanford Bateleur inayorekodi mtetemo katika kina kifupi cha maji. PICHA NA RAMADHANI ALI MAELEZO .



Hivyo makala MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR

yaani makala yote MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/meli-ya-kurekodi-mtetemo-ya-kina-kifupi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR"

Post a Comment