BARAZA MADIWANI KISHAPU LAKUTANA

BARAZA MADIWANI KISHAPU LAKUTANA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BARAZA MADIWANI KISHAPU LAKUTANA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BARAZA MADIWANI KISHAPU LAKUTANA
kiungo : BARAZA MADIWANI KISHAPU LAKUTANA

soma pia


BARAZA MADIWANI KISHAPU LAKUTANA

Na Robert Hokororo, Kishapu

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limekutana kwa ajili ya kuwasilisha na kupokea taarifa za miradi ya maendeleo ya kata zake mbalimbali.

Katika kikao hicho cha kujadili taarifa za robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Boniphace Butondo aliipongeza Kishapu kwa kupata hati safi kutokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu (CAG).  Butondo ambaye pia ni diwani wa kata ya Lagana aliwataka madiwani waendelee kushikamana na kuwahudumia wananchi katika kata zao ili kuleta maendeleo katika halmashauri ya wilaya hiyo.

Alisema ni wajibu wao kuwahamasisha wananchi kuchangia maendeleo katika kata zao sambamba na kuendelea kuwahamasisha kuhusu kilimo hususan cha mazao yanayostahimili ukame.

“Waheshimiwa tuwahudumie wananchi katika kata zetu na hasa ukizingatia hivi sasa Serikali inapigania katika kufufua zao la pamba katika wilaya yetu nasi tuwahamasishe kulima,” alisema.

Aliongeza kuwa katika kikao hicho Baraza linajipima wapi wamefikia katika miradi ya maendeleo na wapi wamekwama hivyo kuweza kutatua changamoto hizo na hatimaye kusonga mbele.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa za kata.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akifungua kikao cha Baraza la Madiwani katika ukumbi wa halmashauri.
Madiwani wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao hicho.


Hivyo makala BARAZA MADIWANI KISHAPU LAKUTANA

yaani makala yote BARAZA MADIWANI KISHAPU LAKUTANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BARAZA MADIWANI KISHAPU LAKUTANA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/baraza-madiwani-kishapu-lakutana.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BARAZA MADIWANI KISHAPU LAKUTANA"

Post a Comment