Samia Suluhu mgeni rasmi Uzinduzi wa Kampeni ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga Dodoma

Samia Suluhu mgeni rasmi Uzinduzi wa Kampeni ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga Dodoma - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Samia Suluhu mgeni rasmi Uzinduzi wa Kampeni ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga Dodoma, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Samia Suluhu mgeni rasmi Uzinduzi wa Kampeni ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga Dodoma
kiungo : Samia Suluhu mgeni rasmi Uzinduzi wa Kampeni ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga Dodoma

soma pia


Samia Suluhu mgeni rasmi Uzinduzi wa Kampeni ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga Dodoma


Image result for picha za sa makamu wa rais samia suluhu
Hussein Ndubikile
Mwamba wa Habari
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kupunguza Vifo vitokanavyo na Uzazi na watoto wa wachanga itakayofanyika mjini Dodoma Novemba 6 mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Mradi- Uzazi Salama, Dkt Phineas Sospeter wakati wa Semina iliyoshirikisha wanahabari yenye lengo la kuhamasisha jamii kuhusu kupunguza vifo vya uzazi na watoto wa wachanga.
Amesema kuwa siku ya uzinduzi viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa mikoa watasaini mikataba ya uwajibikaji na utekelezaji na kwamba kampeni imelenga kupunguza vifo hivyo kutoka 556 katika vizazi hai 100000 kufikia 292 katika vizazi hivyo ifikapo mwaka 2020.
“Huduma za afya zimeboreshwa kwenye vituo vya afya, zahanati na hospitali lakini bado vifo havipungui ndio maana kampeni hii mahsusi inakuja kupambana na tatizo hili, “ amesema.
Amebainisha kuwa vifo vitokanavyo  na uzazi na watoto wachanga husababishwa na mambo mbalimbali yakiwemo ya kutokwa damu kabla na wakati wa kujifungua, kifafa cha mimba, kuharibika kwa mimba, uchungu pingamizi, uambukizo pamoja na magonjwa ya malaria, Ukimwi na upungufu wa damu.
Amessisitiza kuwa katika suala la kuchangia damu wanawake  hawashiriki kikamilifu ambapo asilimia 70 ya kundi hilo hawachanganii hali inayochangia vifo wakati wa kujifungua.
Amefafanua kuwa takwimu zinaonyesha mikoa ya Kanda ya Ziwa, Tabora na Kigoma ndio inayoongoza kwa vifo vitokanavyo na uzazi na huku akiwahimiza wanawake kuwanyonyesha watoto kwa miezi sita.
Amewaomba wanahabari kusambaza taarifa za kampeni hiyo, kusisitiza ushiriki wa wanaume katika uzazi wa mpango na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa afya ya uzazi.
Kwa upande wake, Mratibu wa Huduma za Afya, Said Makora amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo tayari watoa huduma za afya 9000 wameshaanza kazi na kwamba lengo ifikapo mwaka 2020 wafikie 20,000 wawili katika kila kijiji na wilaya.
Katika hatua nyingine, amesema kuwa Halmashauri ya Ulanga, mkoani Morogoro imeshaajiri watoa huduma za afya na kwamba haina tatizo hilo.


Hivyo makala Samia Suluhu mgeni rasmi Uzinduzi wa Kampeni ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga Dodoma

yaani makala yote Samia Suluhu mgeni rasmi Uzinduzi wa Kampeni ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga Dodoma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Samia Suluhu mgeni rasmi Uzinduzi wa Kampeni ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga Dodoma mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/samia-suluhu-mgeni-rasmi-uzinduzi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Samia Suluhu mgeni rasmi Uzinduzi wa Kampeni ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga Dodoma"

Post a Comment