MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA

MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA
kiungo : MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA

soma pia


MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA


Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

KUFUATIA operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu ndani ya Ziwa Tanganyika inayoendelea Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameteketeza zana mbalimbali za uvuvi haramu zenye zaidi ya shilingi bilioni tatu zilizokuwa zikitumika katika ziwa Tanganyika.

Akiongea na wananchi baada ya zoezi la kuteketeza zana hizo haramuza uvuvi katika eneo la Businde nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mpina amewataka wananchi kushirikiana na serekali kwa kuwafichua wahalifu wanaotumia zana haramu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupigwa faini na kwenda jela.

Alisema serekali haitomuonea mtu yoyote huruma ambayeatakamatwa anafanya uvuvi haramu au kuwa na zana za uvuvi haramu awe kiongozi au raia wa kawaida sheria lazima ichukue mkondo wake.''Sisi lengo letu ni kuona samaki wanaongezeka katika ziwa Tanganyika,na watu wavue kwa kufuata sheria ili Taiafa lipate mapato na watu wapate ajira"alisema

Alisema oparesheni inayofanyika katika ziwa Tanganyika ni oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo itaendelea katika maeneo yote ya ziwa Tanganyika lengo likiwa ni kuondoa uvuvi haramu na mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia samaki wachanga na utoroshwaji wa samaki na mazao yake kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Alisema takwimu zinaonyesha utoroshwaji wa samaki na dagaa kwenda nje katika ZIwa Tanganyika ilikuwa ni mkubwa kwenda nje ya nchi bila kulipa chochote na wageni nao kutoka nchi za jirani wanakuja kwenye maji yetu wanavua na kuondoka.
 Waziri wa Mifugo na Uvivu Luhaga Mpina akiteketeza nyavu 352 haramu za uvuvi katika eneo la Businde nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji zilizokamatwa kwenye oparesheni maalum ya kuzuia uvuvi haramu ndani ya ziwa Tanganyika.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiongea na wavuvi pamoja na wafanyabiashara wa mazao ya dagaa na samaki katika mwalo wa Kibirizi kabla ya kuteketeza zana haramu za Uvuvi zilizopatikana kufuatia oparesheni ya kuzuia uvuvi haramu inayoendelea katika Ziwa Tanganyika.



Hivyo makala MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA

yaani makala yote MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mpina-ateketeza-zana-haramu-za-uvuvi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA"

Post a Comment