title : Magereza kumi yateuliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli
kiungo : Magereza kumi yateuliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli
Magereza kumi yateuliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli
Na Mwandishi Wetu
Serikali imeteua jumla ya magereza kumi nchini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli la kulitaka Jeshi la Magereza litumie rasilimali watu ya wafungwa kuzalisha mazao kwa ajili ya biashara na chakula badala ya serikali kuingia gharama ya kulisha wafungwa.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa agizo hilo katika Gereza la Kwamngumi wilayani Korogwe ,mkoani Tanga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema utekelezaji huo unaenda sambamba na uteuzi wa magereza kumi ya kilimo nchini na akiweka wazi uwapo wa mpango maalumu wa kutathmini na kupima mpango mkakati huo kwa kila gereza.
Aliyataja magereza hayo kuwa ni Songwe (Mbeya), Kitai (Ruvuma), Ludewa (Njombe), Mollo (Rukwa), Kitengule (Kagera) ambayo yameteuliwa kulima mahindi, mengine ni Idete na Kiberege (Morogoro) yaliyoteuliwa kulima mpunga huku Kitete (Rukwa), Kitengule (Kagera) na Gereza la Arusha yakiteuliwa kulima maharagae
“Tunahitaji matumizi sahihi ya rasilimali watu na ardhi tuliyonayo katika magereza yetu itumike ipasavyo kwa shughuli za uzalishaji ili tuweze kutekeleza amri ya Mheshimiwa Rais, huku lengo la wizara kupitia jeshi la magereza ni kuweza kuwekekeza fedha kwa kulitumia shirika la uzalishaji mali lililopo ndani ya jeshi hilo na ikiwezekana hapo baadae tuweze kutafuta wateja watakaonunua mazao yatakayozalishwa katika mashamba hayo,” alisema Masauni
Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Gereza la Kwangumi, Christopher Mwenda, alisema wao kama uongozi wa gereza hilo wamejipanga vizuri katika utekelezaji wa aguzo hilo huku akiiomba wizara kuongeza vifaa vya kilimo ili waweze kuzalisha kwa kiwango kikubwa zaidi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa tofali linalotengenezwa na wafungwa ikiwa ni mpango wa uongozi wa gereza la Kwamngumi kukabiliana na changamoto ya makazi kwa askari, Kulia ni Mkuu wa Gereza hilo,Christopher Mwenda, lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa nyumba iliyojengwa na matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamngumi lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo, Christopher Mwenda.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia tofali ambazo zimetengenezwa na wafungwa wa Gereza la Kwamngumi, ambazo hutumika kujengea nyumba za askari ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji na kilimo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa Kaunda suti), na ujumbe alioongozana nao wakipita mbele ya nyumba iliyojengwa kwa kutumia matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamgumi lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hivyo makala Magereza kumi yateuliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli
yaani makala yote Magereza kumi yateuliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Magereza kumi yateuliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/magereza-kumi-yateuliwa-kutekeleza.html
0 Response to "Magereza kumi yateuliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli"
Post a Comment