SIMBA, YA PATA USHINDI KWA UTATA.

SIMBA, YA PATA USHINDI KWA UTATA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SIMBA, YA PATA USHINDI KWA UTATA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SIMBA, YA PATA USHINDI KWA UTATA.
kiungo : SIMBA, YA PATA USHINDI KWA UTATA.

soma pia


SIMBA, YA PATA USHINDI KWA UTATA.

Na David Nyembe, MBEYA
SIMBA SC imerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. 
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ahmed Kikumbo aliyesaidiwa na Omari Juma wote wa Dodoma na Michael Mkongwa kutoka Njombe, Simba ilipata bao hilo kipindi cha kwanza, likifungwa na winga, Shiza Ramadhani Kichuya. 
Kichuya alifunga bao hilo dakika ya saba baada ya mabeki wa Mbeya City kusita kumdhibiti wakidhani ameotea kufuatia pasi ndefu ya juu ya kiungo Jonas Mkude. 


Kiungo wa Simba, Jonas Mkude akikamiliaba na wachezaji wa Mbeya City

Mbeya City walifumuka baada ya bao hilo na kuanza kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba, lakini safu ya ulinzi ya Wekundu wa Msimbazi ikiongozwa na beki Mganda, Juuko Murshid ilisimama imara kuondosha hatari zote.
Sifa zaidi zimuendee mlinda mlango, Aishi Salum Manula aliokoa michomo yote iliyoelekezwa langoni mwake.
Hata kipa kijana mdogo wa Mbeya City, Fikirini Bakari anastahili sifa kwa kuwazuia Simba kupata mabao zaidi, kwani safu ya ushambuliaji ya Wekundu wa Msimbazi ikiongozwa na Mganda, Emmanuel Okwi aliyecheza pamoja na John Bocco kipindi cha kwanza kabla ya kuongezewa na Mrundi, Laudit Mavugo kipindi cha pili.
Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe pointi 19 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda kileleni ikiizidi kwa wastani wa mabao tu Azam yenye pointi 19 pia. 
Baada ya mchezo huo, mshambuliaji mkongwe wa Mbeya City, Mrisho Ngassa alilalamikia uchezeshaji wa refa akisema alikuwa anaionea timu yake uwanjani.;
Kwa upande wake, Kichuya alisema hakuona kama alikuwa ameotea wakati anafunga kwa sababu alimzunguka kwa mbele beki wa Mbeya City na kwa ujumla aliridhishwa na uchezeshaji wa refa.
Kikosi cha Mbeya City kilikuwa; Fikirini Bakari, Erick Kyaruzi, Hassan Mwasapili, Ally Lundenga, Sankan Mkandawile, Babu Ally, Mrisho Ngassa, Mohammed Samatta, Mohammed Mkopi/Victor Hangaya dk82, Omary Ramadhani/Iddi Nado dk64 na Eliud Ambokile. 
Simba SC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, James Kotei, Juuko Murushid, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk88, Muzamil Yassin/Laudit Mavugo dk78, John Bocco, Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima/Said Ndemla dk55.


Hivyo makala SIMBA, YA PATA USHINDI KWA UTATA.

yaani makala yote SIMBA, YA PATA USHINDI KWA UTATA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SIMBA, YA PATA USHINDI KWA UTATA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/simba-ya-pata-ushindi-kwa-utata.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SIMBA, YA PATA USHINDI KWA UTATA."

Post a Comment