title : Maelfu wajitokeza kuchunguzwa magonjwa yasioambukiza Muhimbili-Mloganzila
kiungo : Maelfu wajitokeza kuchunguzwa magonjwa yasioambukiza Muhimbili-Mloganzila
Maelfu wajitokeza kuchunguzwa magonjwa yasioambukiza Muhimbili-Mloganzila
Na Neema Edwin
Maelfu ya watu wamejitokeza kupima afya zao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya kisukari duniani, huku Mkurungezi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Lawrence Museru akiwataka Watanzania kujenga tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kubaini kama wana tatizo la kisukari au matatizo mengine ya kiafya.
Katika maadhimisho hayo hadi kufikia saa 7:30 mchana leo, watu 1,150 wamejitokeza kufanya uchunguzi wa macho, uchunguzi wa afya ya kinywa na meno, uchunguzi wa magonjwa ya kisukari, homoni pamoja na shinikizo la damu.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Prof. Museru amesema kati ya watu wazima 100 takribani watu 9 wana ugonjwa wa kisukari na kati ya watu wazima 3 mmoja ana shinikizo la damu. “Tatizo ni kubwa kwani takwimu zinaonyesha kliniki ya kisukari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ina wagonjwa zaidi ya 6000 wanaoudhuria kwa mwaka,” amesema Prof. Museru.
Prof. Museru amesema kwamba moja ya vyanzo vinavyochangia kuongezeka kwa magonjwa yasioambukiza ikiwamo kisukari na presha ni ulaji usiofaa kama kula chakula kuzidi mahitaji ya mwili na hivyo kunenepa, kula mafuta na chumvi zaidi ya mwili, kutokula matunda na mbogamboga kiasi cha kutosha na kula nafaka zilizokobolewa.
Mkurugenzi huyo amesema matumizi ya pombe kupita kiasi, tumbaku na dawa za kulevya, kutofanya mazoezi na msongo wa mawazo pia yanachangia kuongezeka kwa magonjwa yasioambukiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Prof. Lawrence Museru akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kisukari ambayo huadhimishwa Novemba 14, kila mwaka. Maadhimisho hayo yanafanyika katika hospitali hiyo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Mmoja wa wananchi aliyejitokeza kuchangia damu katika maadhimisho ya siku ya kisukari duniani hospitalini hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Museru akionyesha umuhimu wa wananchi kuchunguza afya zao kwenye maadhimisho hayo.
Wananchi wakiendelea kupatiwa huduma ya uchunguzi leo.
Hivyo makala Maelfu wajitokeza kuchunguzwa magonjwa yasioambukiza Muhimbili-Mloganzila
yaani makala yote Maelfu wajitokeza kuchunguzwa magonjwa yasioambukiza Muhimbili-Mloganzila Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Maelfu wajitokeza kuchunguzwa magonjwa yasioambukiza Muhimbili-Mloganzila mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/maelfu-wajitokeza-kuchunguzwa-magonjwa.html
0 Response to "Maelfu wajitokeza kuchunguzwa magonjwa yasioambukiza Muhimbili-Mloganzila"
Post a Comment