title : SMZ Kushughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma na Kutekeleza Mipango ya Kuleta Mabadiliko.
kiungo : SMZ Kushughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma na Kutekeleza Mipango ya Kuleta Mabadiliko.
SMZ Kushughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma na Kutekeleza Mipango ya Kuleta Mabadiliko.
Na Raya Hamad OR-KSUUUB
Imeelezwa kuwa hatua mbalimbali za msingi zimechukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kushughulikia masuala ya Utumishi wa Umma na pia imekuwa ikitekeleza mipango ya kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa pamoja na mafaniko katika maeneo ya uchumi,usimamizi wa fedha ,kuimarisha taasisi za umma na rasilimali watu, huduma za kujamii na miundo mbinu.
Naibu Katibu Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndugu Seif Shaaban Mwinyi anaeshughulikia masuala ya utumishi ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mwelekeo wa mpango wa kuimarisha Utumishi wa Umma Zanzibar.
Ndugu Seif amesema hatua za mpango wa kuimarisha Utumishi wa Umma ni muhimu kwa vile Zanzibar imepata fursa ya kuingia awamu mpya ya utekelezaji,hivyo majadiliano hayo yatajielekeza katika hali halisi ilivyo sasa, changamoto na hatimae kupokea maoni na michango itayosaidia kuzingatiwa katika uandaaji wa program ya pili ya mabadilikoya utumishi wa umma Zanzibar.
Ndugu Seif ameeleza Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar umeweka msisitizo wa kupatikana kiwango cha juu cha utawala bora na kuondokana na umasikini pamoja na kutambua umuhimu wa nafasi ya usimamizi wa Utumishi wa Umma katika kuyafikia malengo ya maendeleo ya Zanzibar.
Pia alikumbushia na kusema kuwa uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2020 na MKUZA mwanzoni mwa mwaka 2000 zilileta hamasa na ari ya kutafuta mabadiliko ya kimaendeleo ikiwemo pia mabadiliko katika Utumishi wa Umma.
Naibu Seif amefafanua mambo ya msingi iliyoisukuma Serikali kutayarisha na kutekeleza Mkakati wa Mabadiliko katika Utumishi wa Umma kuwa ni pamoja na kuwepo kwa ishara zilizoleta changamoto kubwa kipindi cha nyuma ambazo zilipelekea kukwamisha utoaji wa huduma kisichoridhisha kwa wananchi katika kuleta ufanisi “suala hili lisipoangaliwa malengo ya maendeleo ya kuondosha umasikini hayataweza kufikiwa ”alisisitiza.
Aidha amesema kutokuwepo kwa mgawanyo wa majukumu ulio muafaka baina ya Wizara na Idara, Taasisi zinazojitegemea za Serikali Kuu kwa upande mmoja , Malaka za Serikali za Mitaa kwa upande mwengine kumeviza uwezo wa vyombo hivi kuwahudumia wananchi ,vile vile uwezo mdogo wa watumishi wa umma, upungufu wa watumishi katika utumishi wa umma,viwango vya maslahi kwa watumishi kutokuwa muafaka , jambo lililofanya watu kutopenda kufanya kazi katika utumishi wa umma.
Nae Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti wa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi Daima Mohamed Mkalimoto amesema madhumuni ya kikao hicho ni kutafakari kwa pamoja juu ya utekelezaji wa mpango wa kuimarisha Utumishi wa Umma Zanzibar na kuelezea hali halisi ilivyo kwa sasa changamoto na hatimae kupokea maoni na michango itakayosaidia kuzingatiwa katika uandaaji wa program ya pili ya mabadiliko ya Utumishi wa Umma.
“Tukiwa ni watumishi wa Umma tunajukumu la kufanya kazi kwa kufuata Sera yetu inayotuongoza hivyo kufanyakazi kwa uhakika kutaleta mageuzi” alisisitiza na kusema kuwa Sera inatamka Dhima ya Utumishi wa Umma Zanzibar ni kutoa huduma bora kwa ufanisi na tija kwa umma wa Zanzibar na kwa kiwango cha juu cha uadilifu na heshima.
Baadhi ya mada zilizojadiliwa ni pamoja na usimamizi wa rasilimali watu, usimamizi wa kumbukumbu na taarifa , serikali za mitaa
Hivyo makala SMZ Kushughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma na Kutekeleza Mipango ya Kuleta Mabadiliko.
yaani makala yote SMZ Kushughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma na Kutekeleza Mipango ya Kuleta Mabadiliko. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SMZ Kushughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma na Kutekeleza Mipango ya Kuleta Mabadiliko. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/smz-kushughulikia-masuala-ya-utumishi.html
0 Response to "SMZ Kushughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma na Kutekeleza Mipango ya Kuleta Mabadiliko."
Post a Comment