NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA

NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA
kiungo : NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA

soma pia


NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA

 Na Felix Mwagara, MOHA-Kasulu 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari Polisi kutoza fedha kwaajili ya huduma ya dhamana kwa watuhumiwa waliopo mahabusu katika vituo vya polisi nchini. 
Waziri Lugola pia alisema dhamana hizo zinapaswa kutolewa saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko. 
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Basanza wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, leo, Waziri Lugola alisema ni marufuku kwa askari yeyote atakayeshindwa kutoa dhamana kwa kosa ambalo lina dhamana. 
“Hii tabia sijui imetoka wapi ambayo imejengeka kwa baadhi ya askari polisi, eti mtu akiingia mahabusu ya polisi siku ya Ijumaa ikifika siku ya Jumamosi na Jumapili hawatoi dhamana wakisema dhamana mpaka Jumatatu, hii tabia sio sahihi na ife haraka iwezekananavyo,” alisema Lugola. Lugola aliwataka wananchi nchini kuhakikisha wanaripoti matukio ambayo yanavunjwa na baadhi ya polisi hao ambao wengi wao wanatengeneza mazingira ya rushwa. 
“Kuna tabia ambayo imezoelewa katika jamii, eti kuingia polisi ni bure ila kutoka ni fedha, hii kauli nataka ife, kwasababu nawajua polisi na hawanidanyi kwa lolote, hivyo ole wao ambao watawanyanyasa wananchi kuwaomba fedha,” alisema Lugola. 
Lugola alisisitiza kuwa, dhamana ni haki ya mtu endapo hilo kosa linadhaminika hivyo mwanachi yeyote atakaeombwa fedha anapaswa kuripoti tukio hilo kwa viongozi wa polisi ili polisi achukuliwe hatua za kinidhamu. 
Aidha, Waziri Lugola aliwataka maaskari wa usalama barabarani kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa weledi na si kuwaandikia makosa madereva kwa kuwakomoa endapo magari yao yanamakosa. “Gari likiwa na kosa liandikiwe faini, hilo sina shida nalo, lakini utakuta baadhi ya askari wanaandika makosa mengi ili watengeneze mazingira ya rushwa, hii ssi sahihi ” alisema Lugola.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimsikiliza mwananchi wa Kijiji cha Basanza Wilayani Uvinza, mkoa wa Kigoma, alipokua aamuuliza maswali, baada ya Waziri huyo kuwataka wakazi wa kijiji hicho kutoa kero mbalimbali zinawakabili wilayani humo. Lugola pia alisema dhamana hizo zinapaswa kutolewa saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Mwanamvua Mrindoko alipokua anatoa taarifa yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya.  Lugola aliwataka Polisi nchini watoe dhamana saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwa sababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Mwanamvua Mrindoko (kushoto) alipokua anatoa taarifa yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya. Katika hotuba yake kwa maafisa wa Wilaya hiyo, Lugola aliwataka Polisi nchini watoe dhamana saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Hivyo makala NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA

yaani makala yote NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/news-alert-waziri-lugola-aamuru-polisi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA"

Post a Comment