CLOUDS PLUS, BODI YA FILAMU WAWAKUTANISHA WADAU WA FILAMU KUTAFUTA UBORA.

CLOUDS PLUS, BODI YA FILAMU WAWAKUTANISHA WADAU WA FILAMU KUTAFUTA UBORA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CLOUDS PLUS, BODI YA FILAMU WAWAKUTANISHA WADAU WA FILAMU KUTAFUTA UBORA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CLOUDS PLUS, BODI YA FILAMU WAWAKUTANISHA WADAU WA FILAMU KUTAFUTA UBORA.
kiungo : CLOUDS PLUS, BODI YA FILAMU WAWAKUTANISHA WADAU WA FILAMU KUTAFUTA UBORA.

soma pia


CLOUDS PLUS, BODI YA FILAMU WAWAKUTANISHA WADAU WA FILAMU KUTAFUTA UBORA.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (wapili kutoka kulia) akipata ufafanuzi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi kitengo cha huduma za filamu kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Wilhadi Taipo (wa kwanza kutoka kushoto) wakati akitembelea banda la Bodi ya Filamu Tanzania.
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka Julia) akipewa ufafanuzi kutoka kwa Mhandisi wa masuala ya video na sauti Carlo Cominassi (wa kwanza kutoka kushoto)

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akipewa  ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya utangazaji na filamu kutoka banda la Clouds plus. 
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amewataka waandaji wa vipindi vya luninga, radio na watengenezaji wa filamu nchini kuzingatia maudhui yenye ubora ili waweze kufanikiwa katika soko.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa jukwaa la utangazaji na wasambazaji wa kazi za Sanaa lililoandaliwa na Clouds Plus kwa kushirikiana na Bodi ya filamu nchini Dkt.Mwakyembe amesema kuwa jukwaa hilo liwe endelevu na litoke na majibu yatakayotoa suluhisho ya ya changamoto ya kazi za sanaa zisizo kuwa na ubora.

"Tuone namna tutakavyofanya ili kuweza kikidhi ubora na hatimaye kulishinda soko" amesema Dkt. Mwakyembe.

Dk.Mwakyembe amesema kuwa kuna sababu ya kushawishi kampuni mbalimbali zinazotengeneza vifaa vya kielektroniki vinavyotumika katika utengenezaji wa vipindi na filamu kufunguliwa nchini ili zipatikane bidhaa zenye ubora zaidi.
Dk. Mona Mwakalinga kutoka kitivo cha sanaa na muziki Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amesema kuwa  jukwaa hilo litawasaidia wanafunzi wanaosoma masomo ya uandaaji filamu ,muziki, Habari, mawasiliano na matangazo kufahamu maudhui yanayo hitajika.

"Jukwaa hili la siku tatu litatoa mwanga kwa wanafunzi ambao wanasoma taaluma zinazohusika na utengenezaji wa maudhui kutengeneza programu zenye ubora na jinsi ya kushawishi soko" amesema Mwakalinga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga,  amesema kuwa aliamua kuanzisha Jukwaa hilo kwakushirikiana na Bodi ya Filamu nchini kwakuwa vipindi vingi vya luninga, radio na filamu zinazotengenezwa nchini hazina ubora wakuweza kushindana na soko.
"Tumeona ipo haja kwakuwa tuna uzoefu wa utengenezaji wa maudhui kwa takribani miaka 19 lakini tumeona jambo hili tusilifanye kuwa letu bali liwe la Taifa ndiyo maana tumeishirikisha Wizara na Taasis zake" amesema Kusaga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu nchini Profesa Frowin Nyoni, amesema kuwa uundwaji wa jukwaa hilo utaongeza thamani ya bidhaa za sanaa na kuliingizia Taifa fedha za kigeni.

"Jambo hili liwe endelevu kutokana na umuhimu wake kwa Taifa na uchumi, tutakapo tengeneza bidhaa zenye ubora na zinazozingatia maudhui yenye weledi wa kitaaluma zitauzwa kimataifa na zitadumu na kutumiwa na vizazi vijavyo"amesema Nyoni.
"Jukwaa litaendeshwa mfululizo kwa kipindi cha miaka mitatu kati ya Clouds Media group, Bodi ya Filamu na Wizara ya Habari ,Utamaduni  Sanaa na michezo na kila baada ya mwaka mmoja wa utekelezaji wa wa maadhimiyo kutafanyika tathimini ili kupima ubora wa kazi hizo" amesema.


Hivyo makala CLOUDS PLUS, BODI YA FILAMU WAWAKUTANISHA WADAU WA FILAMU KUTAFUTA UBORA.

yaani makala yote CLOUDS PLUS, BODI YA FILAMU WAWAKUTANISHA WADAU WA FILAMU KUTAFUTA UBORA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CLOUDS PLUS, BODI YA FILAMU WAWAKUTANISHA WADAU WA FILAMU KUTAFUTA UBORA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/clouds-plus-bodi-ya-filamu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "CLOUDS PLUS, BODI YA FILAMU WAWAKUTANISHA WADAU WA FILAMU KUTAFUTA UBORA."

Post a Comment