WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO
kiungo : WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO

soma pia


WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO

*Ni wale washio nje ya kituo, wawe wamehamia ifikapo Desemba 15

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaametoa siku 25 kwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino wanaoishi nje ya kituo chao cha kazi wawe wamehamia.

Pia amemkabidhi Mkuu wa wilaya hiyo Bibi Vumilia Nyamoga orodha ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino ambao wanaishi nje ya kituo cha kazi kwa hatua zaidi. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Oktoba 20, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chamwino.

“Ifikapo Desemba 15 mwaka huu watumishi wote wawe wamehamia katika kituo chao cha kazi. Sheria ya utumishi inamtaka mtumishi aishi katika maeneo ya kituo cha kazi.” Waziri Mkuu amesema lazima watumishi wote wa umma wafuate sheria, kanuni na taratibu za utumishi na atakayeshindwa kuhamia atakuwa amejiondoa kwenye utumishi.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wakuu wa idara na madiwani watambue vyanzo vyote vya mapato. Amesema baada ya kuvitambua wasimamie utaratibu wa ukusanyaji kwa njia ya kielekroniki ili kuiwezesha halmashauri kupanga miradi na kuitekeleza kupitia fedha za ndani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,     Vumilia Nyamoga ordha ya watumishi ambao hawaishi kwenye kituo chao cha kazi cha Chamwino na badala yake wanaishi jijini Dodoma. Alikuwa katika mazungumzo na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmshauri ya wilaya Chamwino kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu) 
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. 



Hivyo makala WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO

yaani makala yote WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/waziri-mkuu-atoa-siku-25-kwa-watumishi_20.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO"

Post a Comment