title : JUMUIYA YA WAAHMADIYYA TANZANIA YAWEZESHA MAJI WAKAZI WA MITAA YA KATA KIHONDA MAGHOROFANI, MANISPAA YA MOROGORO .
kiungo : JUMUIYA YA WAAHMADIYYA TANZANIA YAWEZESHA MAJI WAKAZI WA MITAA YA KATA KIHONDA MAGHOROFANI, MANISPAA YA MOROGORO .
JUMUIYA YA WAAHMADIYYA TANZANIA YAWEZESHA MAJI WAKAZI WA MITAA YA KATA KIHONDA MAGHOROFANI, MANISPAA YA MOROGORO .
Na John Nditi, Morogoro
WANANCHI wa mitaa ya Kata ya Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro wameondokana na adha ya kutopata uhakika maji safi na salama baada kujengwa kituo cha kuchota maji ya bomba kupitia ufadhili wa Jumuiya ya Waislamu Waahamadiyya chini ya mradi wake wa Taasisi ya International Association of Ahmadi Architects and Engineers (I.A.A.A.E).
Mkuu wa Chuo cha Ahmadiyya Muslim Jama’at Tanzania, Sheikh Abid Mahmood Bhatti alisema hayo kabla ya kukaribishwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe , kuzindua mradi wa maji uliojulikana kwa jina la ‘ Water For Life’ katika kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro na jirani zake .
Alisema , Jumuiya hiyo pamoja na kuwa ni taasisi ya kidini , inayo mipango mbalimbali ya kutoa huduma za kijamii zikiwemo katika sekta ya afya, elimu , umeme wa soka na maji.
“ Mradi huu ulianzishwa mwaka jana baada ya kupitishwa na Hadharat Khalifa tul Masih kiongozi mkuu wa Jumuiya ya waislamu waahmadiyya duniani kupitia taasisi ya IAAAE” alisema Bhatti.
Mkuu wa Chuo alisema , jamii ya Kihonda Maghorofani iliyopo karibu na taasisi hiyo wanaweza kuchota maji lita zisizopungua 10,000 kwa siku kwa ajili ya matumizi ya nyumbani .
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( kulia ) akifungua koki ya maji wa ajili ya kujaza ndoo mara baada ya kuzindua mradi wa maji uliojilikana kwa jina la ‘ Water For Life’ hivi karibuni eneo la kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro ambayo yanawanufaisha wa kazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani , iliyopo Manispaa ya Morogoro .
Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania , Tahir Mahmood Chaudhary Sahib ( kulia) akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro, Winifrida Laizer , mara baada ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( hayupo pichani) kuzindua mradi wa maji uliojilikana kwa jina la ‘ Water For Life’ hivi karibuni katika kituo cha Jumuiya hiyo eneo la Kihonda Maghorofani .
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( kulia )akikata utepe kuashiria kuzindua mradi wa maji uliojulikana kwa jina la ‘ Water For Life’ hivi karibuni eneo la kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro ambayo yanawanufaisha wa kazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani , iliyopo Manispaa ya Morogoro na ( wa kwanza kulia ) ni Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania , Tahir Mahmood Chaudhary Sahib.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( wapili kulia ) akioneshwa kisima cha maji na mkuu wa Chuo cha Ahmadiyya Morogoro , Sheikh Abid Mohmood Bhatti ( kushoto) kabla ya kuzindua mradi wa maji uliojulikana kwa jina la ‘ Water For Life’ hivi karibuni eneo la kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro ambayo yanawanufaisha wa kazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani , iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Baadhi ya wakazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro wakichota maji safi na salama ya bomba mara baada ya Mkuu wa mkoa , Dk Kebwe Stephen Kebwe , kuzindua mradi wa maji uliojilikana kwa jina la ‘ Water For Life’ hivi karibuni eneo la kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Internatioal Association of Ahmadi Architects and Engineers (I.A.A.A.E) Akram Ahmadi Sahib ( kulia) akiwa ameongozana na mmoja wa viongozi wa Ahmadiyya Muslimu Missionaries Training Centre iliyopo kata ya Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro wakitoa kuangalia mtambo wa kusukuma maji kwa kutumia umeme wa jua. (Picha na John Nditi).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala JUMUIYA YA WAAHMADIYYA TANZANIA YAWEZESHA MAJI WAKAZI WA MITAA YA KATA KIHONDA MAGHOROFANI, MANISPAA YA MOROGORO .
yaani makala yote JUMUIYA YA WAAHMADIYYA TANZANIA YAWEZESHA MAJI WAKAZI WA MITAA YA KATA KIHONDA MAGHOROFANI, MANISPAA YA MOROGORO . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JUMUIYA YA WAAHMADIYYA TANZANIA YAWEZESHA MAJI WAKAZI WA MITAA YA KATA KIHONDA MAGHOROFANI, MANISPAA YA MOROGORO . mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/jumuiya-ya-waahmadiyya-tanzania.html
0 Response to "JUMUIYA YA WAAHMADIYYA TANZANIA YAWEZESHA MAJI WAKAZI WA MITAA YA KATA KIHONDA MAGHOROFANI, MANISPAA YA MOROGORO ."
Post a Comment