title : AZAM FC KESHO KUIKARIBISHA SINGIDA UNITED CHAMAZI
kiungo : AZAM FC KESHO KUIKARIBISHA SINGIDA UNITED CHAMAZI
AZAM FC KESHO KUIKARIBISHA SINGIDA UNITED CHAMAZI
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC kesho itawakaribisha Singida United ya mkoani Singida kwenye mchezo wa raundi ya pili ya michuano wa kuania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mchezo huo utachezwa uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam saa moja usiku ambapo AzamFc watakuwa wenyeji wa Singinda United katika mchezo huo.
Akizungumza leo Dar es Salaam,Ofisa Habari wa Azam FC Jaffary Maganga amesema mchezo huo ni mgumu ukizingatia na kikosi cha Singida kipo vizuri ila watahakikisha watapambana ili kushinda mchezo huo.
"Kikubwa sisi kwetu ni kupambana ukizingatia timu zote mbili zina upinzani wa hali ya juu na kila mmoja anataka kuibuka kidedea katika mchezo huo na ukizingatia Ligi inaelekea mwishoni"amesema Jaffary.
Amesema nyota wao wa kimataifa Daniel Amor ataukosa mtanange huo pamoja na Waziri Junior aliyefanyiwa upasuaji wa paja kwa sasa anayefanya mazoezi madogo madogo na kuongeza Nahodha wa kikosi hicho Himidi Mau yupo fiti na kesho atacheza mechi ya kesho dhidi ya Singida united.
"Mchezaji wetu Himidi Mau alianza mazoezi na wenzake wiki yote hii na anaendelea vizuri, kurejea kwa kiungo huyo katika kikosi kutaleta morali katika timu na imezidi kuongeza nguvu na tutapambana katika Uwanja wetu wa Nyumbani katika kuhakikisha tunapata pointi 3,"amesema Jaffary.
Hivyo makala AZAM FC KESHO KUIKARIBISHA SINGIDA UNITED CHAMAZI
yaani makala yote AZAM FC KESHO KUIKARIBISHA SINGIDA UNITED CHAMAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AZAM FC KESHO KUIKARIBISHA SINGIDA UNITED CHAMAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/azam-fc-kesho-kuikaribisha-singida.html
0 Response to "AZAM FC KESHO KUIKARIBISHA SINGIDA UNITED CHAMAZI"
Post a Comment